Viongozi Simba, mpeni timu Hassan Dalali, 'Field Marshal' awakomeshe Utopolo Jumapili

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Nawashauri viongozi wa Simba, mechi yetu na Utopolo safari hii tuache mzaha, tumefuzu group stage lkn furaha yetu kuelekea krismas ni kumuua utopolo tu, haiingii akilini kila tunapocheza nao wanatudhalilisha kwa mabao ya kitoto, mtu pekee mwenye ujanja wa kuikomesha Utopolo ni Hassan Dalali pekee, acheni dharau, Utopolo kiboko yao ni Dalali tu, alikuwepo marehemu Juma Salum, amir Bamchawi na msukuma Marco Masanja ambaye yuko jela China, otherwise mtawapa cha kusema hao watu.

Chonde chonde, wasaliti wote msiwashirikishe kwenye timu yetu kuelekea jumapili, hasa huyo mwanasiasa wa kusini.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Kwani mechi walizoshinda yanga dhidi ya simba Dalali alikua nje ya nchi??
 
Unataka kurudisha nyuma maendeleo ya timu. Zama za kuruka ukuta tumewaachia Yanga na ona wanavyoteseka. Uchawi siyo dili.
 
Havina umuhimu kwetu
Acheni wazee wapumzike
 
Aina haja,atuna presha na mechi ya j'pili watagongwa tu palepale walipo jeruhiwa na washkaji zake Simba Al hilal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…