Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Heshima zinazotolewa kwa viongozi wakuu wa Taifa letu waliotangulia mbele ya haki zinataka kutujengea taswira kwamba flani ni muhimu kuliko flani Jambo ambalo hatukuliona walipokuwa hai. Namna tulivyoziandaa nyumba zao za kudumu Kuna utofauti mkubwa Sana, namna tunavyowazungumzia upo utofauti mkubwa pia. Kisaikologia tunaweza kusema hatusukumwi na usawa wa hadhi zao Bali tunasukumwa na nafsi ya urafiki baina yetu na wao.
Mizimu yao inatusumbua, upendeleo wa wazi katika kuwahudumia unaonekana kuonyesha yule ni Bora kuliko huyu. Pls tutafakari kuhusu namna Bora ya kuwakumbuka Hawa watu,tujitathimini namna ambavyo jamii zinazowazunguka huko Butihama, Mtwara na Geita zitapata miradi na miundombinu kwa usawa. Tunaposahau Butihama kwa zaidi ya miaka 20, tukasahau Mtwara kwa miaka miwili plus na kupakumbuka Geita miezi sita tunajenga picha kwamba huyu na yule Wapo tofauti.
Tusipoweka usawa wa kisheria na kuusimamia tutawabagua hata watoto na familia zao, tusiwahudumie kwa ukaribu wetu nao Bali tuwahudumie kwa mujibu wa sheria. Tukizima mwenge huku basi next time tukazime kule na ijulikane wazi kwamba sheria inatamka hivyo.
Tukijenga kilomita moja ya lami kule na huku itamkwe moja kuwaenzi. Tukijenga kituo Cha afya na kule tujenge ili wananchi wajue wazi kwamba eneo lao likito Rais Basi watapata miradi na hudumu zifuatazo ikiwa ni kumuenzi Mtoto wao.
Nje ya hapo miradi mingine ibaki kutolewa kupitia mgao wa kawaida usio na upendeleo