Kumbe kuna thread kama Hii?Kuna watu wako hapa kutekeleza miradi ya watu kwa maslahi wanayojua wenyewe,Ni muda mrefu kidogo tangu niingie hapa kutokana na Majukumu,nawashukuru sana Marafiki zangu wa JF kwa kunipa Taarifa juu ya kinachoendelea.Naomba nijibu japo kidogo na kwa ufupi,ingawa najua naweza nisikutosheleze
Nuclear1,
Naomba upate mda uje hapa kuthibitisha tuhuma Hizi ulizotoa hapa,nina uhakika hauna Envedence na sijui Lengo lako ni nini.Mwaka jana ulikuja na thread nyingine za uongo na uchafu mwingi tu kwa malengo unayoyajua
Umeongelea kwamba natoka Kilimanjaro,Sikatai.Mimi ni mzaliwa wa Kilimanjaro kweli.Je,hilo ni kosa kugombea uongozi ndani ya BAVICHA?Ni lini tulianza kuchagua watu kwa kutumia makabila yao au Dini zao?Haya si mamabo ya kujadili kwa sasa,na hayana Tija.
Kuhusu Kuhusika kwangu ku-incite vurugu katika uchaguzi wa serikali za wanafunzi chuoni kwetu,huu ni uongo.Polisi India wangenikamata na kunifungulia Mashtaka.Ni very simple,Njoo uthibitishe hili tafadhali
Kuhusiana na uchaguzi wa Acharya,mimi nilikuwa na haki ya kumpigia kampeni mgombea ambaye angeshinda kule ili tufanye nae kazi kwa urahisi.kipindi kile hatukuwa na uhusiano mzuri na ubalozi wetu hiyo hali tuliikuta.Ubalozi ulikuwa unatumia kugawanyika miongoni mwetu ili wasiwajibike kutuhudumia,kwa hiyo ilikuwa ni lazima tuungane tuwe kitu moja ili kutetea maslahi ya wanafunzi wenzetu.Tusingekubali kuishi kama wakimbizi,huku tukiwa na ubalozi ambao unalipwa kwa kupitia kodi ya Watanzania.Watanzania mlio nje ni mashahidi wa jinsi balozi zetu zinavyopenda kusukumwa katika kutekeleza wajibu wao.Ikumbukwe,Balozi ni mwakilishi wa Rais nje ya nchi.Ubalozi unajukumu la kusimamia Maslahi ya watanzania nje ya nchi.
Kuhusu Kugombea Uongozi wa serikali ya wanafunzi wa kimataifa,Naona pia unapotosha.Mtindo wangu wa kampeni ulikuwa ni kutafuta washirika ambao wangenipigia kampeni.Kila nchi nilihakikisha na kuwa Mshirika mwenye ushawishi bila kujali kabila,dini au class.Sioni kosa lolote nililofanya
Kuhusu kugombana na Profesa,hilo ni suala la uwongo.Nilihitaji clarifications,argument ikahusisha Darasa Zima.Kama ni ugomvi ulitokea katika sura nyingine na ilikuwa ni Darasa vs profesa wao.Hii ni hoja ya kitoto mno
Umeongelea kuhusu kumkataza balozi asijihusishe na matawi ya vyama vya siasa.Ndiyo nakubali nilifanya hivyo,kwa kuwa mimi naamini Watanzania tulikuwa wachache sana nje.tulitakiwa kuishi kwa umoja wetu.Hata mimi sikufungua Tawi la CHADEMA kwa kuwa niliamini kabisa kwa kufanya hivyo tunarudisha nyuma au kufifisha spirit ya umoja wetu kama Watanzania.Balozi ni wa Watanzania,si wa wana-ccm wala Cuf,wala CHADEMA.
Tafadhali naomba uache kupotosha kwa kutumia jina la uongo,njoo hapa uongee ukweli.Halafu unadiriki kuji-associate na CHADEMA na wakati tunajua wewe ni CCM Damu Damu. Kaeni muimarishe chama chenu,kachukue fomu za UVCCM pia mwakani kama umri wako utakuwa unaruhusu,vinginevyo subirini tuongoze BAVICHA,Mtaona cha mtema kuni.Stop Hating brother!