MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi.
Mwaka 2012 kulitokea jambo la kushangaza sana ndani ya CHADEMA lakini kama kawaida makada wa Chama Cha Mbowe walitetea na kutukana mno yeyote aliyekuwa na maoni tofauti. Ilikuwa ni kujulikana kwamba bado aliyekua katibu mkuu wa CHADEMA Dr Slaa kwamba anamiliki kadi ya chama pendwa CCM. Lilikuwa jambo la kushangaza kwasababu tumeona mara zote watu wanapojiunga na chama kingine hurudisha kadi zao za vyama wanavyotoka na kupewa kadi mpya. Wengine waliochefukwa hufikia kuchoma kadi za vyama walivyovichoka. Lakini bosi wa CHADEMA akawa bado ana kadi ya CCM. Watu wenye akili wakasema bado Dr Slaa ana mapenzi makubwa kwa CCM ila wafuasi hoyahoya walimtetea. Miaka kadhaa baadae Dr Slaa akaja kufanya kazi ndani ya serikali ya CCM kama balozi kwa uaminifu uliotukuka.
Msingi wa stori ya Slaa ni kujikumbusha tulikotoka ili tusije tukaona hawa viongozi wa sasa hivi wa CHADEMA kwamba wanafanya maajabu. Kuna tabia inayoshangaza sana kwa viongozi waandamizi wa CHADEMA kutoa matamko mitandaoni kuhusiana na ishu za ndani ya CCM. Kwa mfano kwenye ishu ya Polepole na chama chake tumeona makada wakubwa wa CHADEMA wakishauri mambo mbalimbali hasa demokrasia ndani ya CCM huku wengine wakienda mbali zaidi kutaka Polepole atendewe haki. Yaani hapa bila kujijua ni kwamba hawa viongozi wa Chama Cha Mbowe wanaipigania CCM iwe sawa. Mimi nimehisi mambo mawili; labda huenda viongozi wa CHADEMA kimoyomoyo wanakubaliana na kauli ya Mwalimu Nyerere kwamba bila CCM imara hakuna Tanzania imara au wao pia ni kama Dr Slaa kwamba wana kadi za CCM kisirisiri.
Viongozi wa CHADEMA hasa hawa wakubwa jitahidini kutoongea ovyoovyo hasa mitandaoni. Kwani hamuoni kina Chongolo na Mangula wako bize na CCM yao bila kuongelea kila tukio? Mnakiua chama chenu kwa mambo ya ovyo. Msipuuze huu ushauri wa bure.