Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Singida, wameangua kilio kwa kumwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atoe tamko la kuachiwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho ambaye anadaiwa kukabiliwa na kesi ya uhani.
Viongozi ambao ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Singida, Omary Toto, Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Kati, Jackson Jingu na wanachama wengine, wametoa ombi hilo kwa nyakati tofauti wakati walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari na kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Standi ya zamani Singida Mjini.