#COVID19 Viongozi wa CHADEMA wanahamasisha chanjo ya Corona ila hatuwaoni wakichanjwa

#COVID19 Viongozi wa CHADEMA wanahamasisha chanjo ya Corona ila hatuwaoni wakichanjwa

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Ndugu zangu Watanzania. Wakati Bwana Yesu yuko duniani aliwaeleza wafuasi wake kuwa Mafarisayo wameketi kwenye kiti cha Nabii Musa. Wasikilize maneno yao ila wasienende kwa mfano wa Matendo yao.

Leo hii maneno hayo yanatimia kwa Viongozi wa Chadema.

Wamekuwa wakihamasisha sana juu ya chanjo. Kiasi cha hadi kufikia Mwenyekiti wao Ndugu Freeman Mbowe akamsihi Mh. Rais, Mama yetu Samia Suluhu Hassan aondoe hiyari aliyotuwekea na wote tukamatwe na tuchanjwe kwa lazima.

Msimamo huo umeendelezwa na viongozi wengi akiwepo Mch. Msigwa na wenzie wengi ndani ya Chadema. Na tofauti na Chama Cha Mapinduzi, ambapo wanachama wake wengi wanashauri vinginevyo. Lakini ndani ya Chadema viongozi na wanachama wote ni kama wamekubaliana tupige chanjo maana sijaona hata Mwenyekiti wa chadema wa Tawi au mwanachama akisema chanjo haifai.

Sasa changamoto yangu inakuja, toka chanjo iingie nchini na kuzinduliwa na Mama yetu, Mh. Rais, sijaona kiongozi hata mmoja wa chadema wala tisheti hata moja ya M4C ikienda kuchanjwa.

Mafarisayo walikuwa na maneno mazuri wakimfuatisha Musa ila matendo yalikuwa opposite.

Chadema wana maneno mazuri kuhusu chanjo wanazohamasisha lakini kwenye kuchanjwa hawatingi.

Na waswahili wanasema Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.

Je, tuamini lipi kati ya haya?

1. Viongozi wa Chadema wamepigwa posho waipigie chanjo upatu lakini hawaiamini?

2. Viongozi wa Chadema na wanachama wao wako radhi kufa na Corona kuliko kwenda kuchanja na kujikinga?

3. Viongozi wa Chadema wanalenga kuwafurahisha wadhamini wao kwa kuwapotosha Watanzania?

Jamani naomba mnisaidie.
 
Walisha chamjwa nje ya nchi
Tunataka kuona picha wakichanjwa au vyeti.aliyekiri kuchanjwa ni Mbowe tu. Hata Lissu na Lema wanaoishi huko hawajawahi kusema wamechanjwa.
 
Haya mzee jongwe
Screenshot_20210805-163224_Instagram.jpg
 
Mtoa hoja umeambia chanjo ni HIARI yako na sio ya lazima,na acha UONGO Mr.Mbowe hakutamka watu wakamatwe ili wapate vaccine,na usituletee familia inayokua kwa kuamini UONGO.
 
Nini maana ya kufanya chanjo kuwa ya lazima? Atayekataa lazima maanake nguvu itumike. Bwashee vitu vidogo hujui?
 
Back
Top Bottom