PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Zikiwa zimebaki siku sita kufanyika uchaguzi mkuu, zaidi ya viongozi 200 wa dini wa mikoa ya kanda ya kaskazini wameonyana, asitokee wa kuvuruga amani ya nchi.
Akizungumza Oktoba 22, 2025 katika semina ya amani iliyofanyika Moshi Mjini, ikiwahusisha viongozi wa dini mbalimbali wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga, Shehe wa Mkoa wa Kilimanjaro, Shaban Mlewa,
amesema uchaguzi unaokuja, usiwafanye kuwa sababu ya wao kupotoka na kupata ghadhabu za Mwenyenzi Mungu, huku wakiomba kila mmoja wao kuchukua jukumu la kuwa walinda amani wa kweli katika vitendo vyao, maneno yao na hata fikra zao.
Aidha, Mshauri wa Baraza la Ulamaa na Shehe wa Mkoa wa Arusha, Shehe Shaban Juma, ameeleza haya: “Kwa hiyo akitokea shehe wetu au mchungaji wetu mkubwa, mazungumzo yake vile unavyoyaona yanapindapinda hayakunyooka katika kuizungumza amani moja kwa moja, kwa upande wetu sisi tuna haki kwa hilo kuacha kumkumbali.
…Basi na ndivyo hivyo hivyo hata akiwepo mwanasiasa mkubwa, alie na uwezo mkubwa wa kisiasa lakini mwisho wa maneno yake yatavunja amani, hatupaswi kuyakubali maneno yake.”