Viongozi wa dini mbioni kukosa uhalali machoni pa waumini wao

Viongozi wa dini mbioni kukosa uhalali machoni pa waumini wao

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Kumekuwa na tabia sugu ya viongozi wengi wa Dini kusoma aya zinazohamasisha tu kutoa SADAKA.

Lakini pia wamekuwa wakibuni mbinu za kila aina za kuwakamua Waumini wao Makanisani.

Mambo ya ovyo yanayofanywa na viongozi wengi wa serikali hawana habari nayo kwa sababu wao wanashibishwa kwa SADAKA, MICHANGO, FUNGU LA KUMI, ZAKA nk. kutoka kwa Waumini wao.

Viongozi hawa wa Dini huji kusikia hata siku moja wanakemea hadharani maovu yanayofanywa na viongozi wengi wa serikali.

Kwa hiyo, kuanzia sasa tunataka viongozi wetu wa Dini waache mara moja kufumbia macho dhuluma zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali kwa wananchi.

Tunataka viongozi wa Dini wawe mstari wa mbele kabisa na wapaze sauti zao waziwazi kukemea maovu yanayofanywa na viongozi wengi wa serikali, baada ya hapo ndipo waje kuomba SADAKA, MICHANGO FUNGU LA KUMI, ZAKA, SHUKRANI nk.

Kama hawatafanya hivyo, automatically watakuwa wamekosa kabisa uhalali machoni pa Waumini wao na kwa sababu hiyo, Waumini hatutakuwa tayari kuimbishwa nyimbo za MICHANGO wakati masuala ya msingi kabisa hayafuatiliwi.

Kwa wakristo tukumbuke hata Yesu aliteswa kwa sababu aliwatetea Waumini kutokana na madhulumu ya viongozi wa serikali.

Viongozi wa Dini jitafakarini kwa kina, kama mmoja wenu ameshindwa kazi ya kuwapigania Waumini kwanza, akae pembeni waje wanaoweza kazi hiyo.
 
Viongozi wa dini wasipokosoa maovu ya serikali ndiyo furaha sana kwa hiyo serikali. Wakiikosoa tu wataambiwa wanachanganya dini na siasa.Na ndipo utajua wanasiasa wanawagwaya watu wa dini kwa kiasi gani!
 
Sikuhizi hakuna viongozi wa dini, kuna wezi na matapeli walio jificha nyuma ya msalaba na msikiti.
 
Usijeneroraiz mkuu! Wataje tu hao viongozi maana ya kwetu yamepangwa mwaka mzima!
 
Viongozi wa dini hawawezi kuwakemea watawala ambao wapo madarakani kwa rushwa ufisadi na kafara
Hizi ni mamlaka mbili zinazolindana na kuendelea kuitafuna nchi na wananchi.
 
Ndo maana skuizi mchungaji pekee namsikiliza Tanzania ni mwakasege tu.hao wengine hapana aise
 
Huko kwa sasa ni janga watu wana linda matumbo yao kwa gharama zozote bora ukaabudu Mbuyu kipindi cha njaa utakula MABUYU na ASALI
 
Wakati ukifika hidi Dini zitakuja kufa kutokana na viongozi wengi wa Dini kupewa chochote na mfumo ili kuyafumbia macha maovu yanayofanywa na viongozi wengi wa serikali.
 
Kumekuwa na tabia sugu ya viongozi wengi wa Dini kusoma aya zinazohamasisha tu kutoa SADAKA.

Lakini pia wamekuwa wakibuni mbinu za kila aina za kuwakamua Waumini wao Makanisani.

Mambo ya ovyo yanayofanywa na viongozi wengi wa serikali hawana habari nayo kwa sababu wao wanashibishwa kwa SADAKA, MICHANGO, FUNGU LA KUMI, ZAKA nk. kutoka kwa Waumini wao.

Viongozi hawa wa Dini huji kusikia hata siku moja wanakemea hadharani maovu yanayofanywa na viongozi wengi wa serikali.

Kwa hiyo, kuanzia sasa tunataka viongozi wetu wa Dini waache mara moja kufumbia macho dhuluma zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali kwa wananchi.

Tunataka viongozi wa Dini wawe mstari wa mbele kabisa na wapaze sauti zao waziwazi kukemea maovu yanayofanywa na viongozi wengi wa serikali, baada ya hapo ndipo waje kuomba SADAKA, MICHANGO FUNGU LA KUMI, ZAKA, SHUKRANI nk.

Kama hawatafanya hivyo, automatically watakuwa wamekosa kabisa uhalali machoni pa Waumini wao na kwa sababu hiyo, Waumini hatutakuwa tayari kuimbishwa nyimbo za MICHANGO wakati masuala ya msingi kabisa hayafuatiliwi.

Kwa wakristo tukumbuke hata Yesu aliteswa kwa sababu aliwatetea Waumini kutokana na madhulumu ya viongozi wa serikali.

Viongozi wa Dini jitafakarini kwa kina, kama mmoja wenu ameshindwa kazi ya kuwapigania Waumini kwanza, akae pembeni waje wanaoweza kazi hiyo.
Usijitoe akili,dini na serikali ni pamde mbili za shilingi ambazo kazi yao ni moja tu kutawala na kumkontrol mwanadamu,

Kuna wale wanajikuta hawali kitimoto ila na fukuana mitaro wao ma wake zao wakisema ni sunna za mtume.
 
Pia waache unafiki wa kujipendekeza kwa serikali. Malasusa na Pengo waamue moja kutumikia CCM au kanisa
 
Waumini ndio wajinga wanadhani viongozi wa dini ni binadamu wasio wa kawaida,,wanaweza kuwaondolea shida zao na kuisema serikali kwa niaba yao.

Ukweli ni kwamba hivyo vitabu vya dini unatakiwa uvisome na uvielewe na uviishi,, wajibu wa kuipongeza au kuikosoa serikali ni wa wananchi wote. Na shida zako ni jukumu lako kupambana nazo kama umeamua kumkabidhi kiongozi wa dini akutatulie ujue hakuna vya BURE.
 
Sawa,mkuu. Nimeamini dini na serikali lao ni moja tu, kumcontrol mwanadamu.
 
Back
Top Bottom