Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 13,864
- 35,079
Viongozi wa dini katika nchi yetu tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa 2020.
Wanasiasa wameshaanza kujipitisha pitisha kwenye nyumba za ibada na kujifanya ni watu wema Sana na kwamba huu ni wakati wa kuwa wamoja na kuongeza upendo.
Inasikitisha kuona kwamba kwa kipindi Cha miaka minne taifa limeshuhudia kutekwa kwa watanzania wenzetu na mbaya zaidi wenye mamlaka wamekaa kimya kabisa hawakemei Mambo haya ambapo kimsingi inaleta tafsiri kwamba wanayabariki.
Sasa viongozi wa dini tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu tunaomba msemee mazingira ya haki yatakayopunguza hujuma dhidi ya wasio na dola ila wana inspire kugombea nafasi mbalimbali.
Uzoefu unaonyesha kipindi Cha uchaguzi kuanzia kampeni mpaka kutangazwa matokeo ni kipindi cha wanasiasa wenye dola kuwahujumu wasio na dola.
Hivyo basi viongozi wa dini mtakaowakaribisha wanasiasa kwenye madhabahu za bwana na nyumba za bwana misikitini na makanisani muwakumbushe kutenda haki muwaambie waache kuwahujumu wasio na dola kwani kwa kufanya hivyo ni machukizo kwa Mungu.
Wanasiasa mjiulize mnawezaje kuingia kanisani na misikitini mnaomba kuombewa halafu kesho mnaenda kutesa na kuteka watu wa Mungu?
Viongozi wa dini kumbukeni Mungu anaona ushirika wenu na wanasiasa nasisi waja wa Mungu tunaona pia .
Mwenye masikio na asikie.