PreGE2025 Viongozi wa Dini Shinyanga Wakemea Ukatili dhidi ya Watu wenye Ualbino Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

PreGE2025 Viongozi wa Dini Shinyanga Wakemea Ukatili dhidi ya Watu wenye Ualbino Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kuelekea katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 viongozi wa Dini mkoani Shinyanga wamekemea vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye Ualibino ikiwemo mauaji ambayo hushamiri wakati wa uchaguzi yahusishwa na imani za ushirikiana kwa dhana potofu ya kupata uongozi.

Tamko hilo limetolewa na Askofu Samawi Alex Samawi katika ibada maalum ya kuwasimika wachungaji wapya 14 wa Kanisa la Ufunuo Tanzania Jimbo la Kahama, ambapo amewataka wachungaji hao kuwa mstari wa mbele kufundisha jamii kuachana na vitendo hivyo ambavyo ni chukizo kwa Mungu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Nao baadhi ya wachungaji waliosimikwa katika kanisa hilo wameahidi kuwa mabalozi wa amani katika maeneo watakayopangiwa kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom