Kuelekea katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 viongozi wa Dini mkoani Shinyanga wamekemea vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye Ualibino ikiwemo mauaji ambayo hushamiri wakati wa uchaguzi yahusishwa na imani za ushirikiana kwa dhana potofu ya kupata uongozi.
Tamko hilo limetolewa na Askofu Samawi Alex Samawi katika ibada maalum ya kuwasimika wachungaji wapya 14 wa Kanisa la Ufunuo Tanzania Jimbo la Kahama, ambapo amewataka wachungaji hao kuwa mstari wa mbele kufundisha jamii kuachana na vitendo hivyo ambavyo ni chukizo kwa Mungu.