Mwana kondoo 2025
JF-Expert Member
- Apr 6, 2025
- 495
- 580
Kwa hali tuliyomo kisiasa kama nchi suala la Haki na Umoja lazima lisemwe kwa pamoja.
Wananchi tumegundua kuna kundi la viongozi wa dini wapigania HAKI kama kipaumbele na kuna kundi lina pigia chapuo AMANI kwanza kwa kuipata kwa hali yoyote ile, kuna kundi la kati linazungumzia UTULIVU zaidi.
Hoja yangu ni kwamba vyama vya siasa vya upinzani vimesimama na HAKI na CCM imesimama na Amani na Utulivu. Ukiangalia kwa kina kimtizamo nchi imegawanyika kwenye makundi makuu mawili na Haki na la Amani na utulivu mgawanyiko huu wa kimtizamo unatoa taswira ya mgandamizwaji(Upande wa HAKI)na mgandamizaji(Mtawala au kimsingi mtetezi wa amani).
Kwa makusudi nadharia hizi mbili zinatenganishwa na kila upande kukidhi maslahi yake na hili limegawa makundi ya viongozi kila kundi na mtizamo wake kwa kusudio lake. Kwa maoni yangu ebu viongozi wote wa dini unganisheni nguvu kudai Haki kwanza itendeke Amani na Utulivu vitakuja vyenyewe tu.
Hivi vitu vinapaswa viwepo kwa pamoja kimchakato Haki kwanza kisha Amani. Na Amani isiyo ya kulazimisha ikishamiri maana yake kutakuwa na Haki inayoonekana ndani yake. Serikali itende Haki, Mahakama zitende Haki, na Bunge kama wawakilishi watende haki kwa wananchi. Taizo kubwa ni siasa na uchaguzi kwa sasa. Tujadili.