Viongozi wa Dini tuwaelimishe viongozi wanasiasa kutosogelea Madhahabu wakati wa Ibada

Viongozi wa Dini tuwaelimishe viongozi wanasiasa kutosogelea Madhahabu wakati wa Ibada

Carica_papaya

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2018
Posts
767
Reaction score
1,272
Viongozi wa dini hasa dini za Kikristo mnaombwa kuwakumbusha viongozi wa kisiasa kuheshimu Mimbari wakati wa ibada.

Mimbari ni sehemu ambayo Walawi wanaruhusiwa kufanya Ibada na matamko yao kama walivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu.

Waislamu wenyewe hili lipo wazi Masheikh ndio huruhusiwa kusimama na kutoa mawaidha. Hii yawezekana na mfumo wao mzuri wa kuwajengea Waumini wao tokea wakiwa wadogo ( Madrassa) kutii Mamlaka na Amri za Mwenyezi Mungu.

Ni muhimu kwa Wenzetu viongozi wa dini za Kikristo kujenga huu utaratibu kwa Waumini kuanzia kwenye Bible sunday schools na Pathfinder. Kwa kuwa viongozi hata wanapopata mamlaka hawataweza kutoa matamko ya kufuru.

Mfano kumfananisha mwanadamu na Mwenyezi MUNGU ambayo ni Kufuru kwa mafundisho ya dini zote.

Soma 2Samwel 6: 6-7 Nini kilimpata Uzzah alietaka kusaidia kushika sanduku la Bwana wakati hii ilikuwa ni kazi ya Walawi.
 
Naunga mkono hoja 💯.

Yaani tumefikia hatua kiongozi tena mkubwa kabisa wa serikali anasimama mbele kwenye mimbari ya dini anatangazia umma kuwa kiongozi aliyeko hoi tena taabani kuwa ni mzima na ana chapa kazi. Hii na dhihaka ya wazi kabisa kwa Mwenyezi Mungu.

Hili naomba lipigwe stop mara moja kwaajili ya kuheshimu nyumba takatifu za Mungu.
 
Mimi huwa nashangaa sana

Mtu kama
1. Waziri mkuu,
2. Nakamu wa Rais,
3. Rais

Wana majukwaa mengi sana nje ya nyumba za ibada kwanini wanapenda kupanda kwenye mimbali ya makanisa na misikiti?

Majukwaa Yao ni haya
1. TBC taifa (radio na television)

2. Waandishi wa habari... mikutano

3. Bunge

4. Mkutano ya kisiasa

5. Wawapo ziarani

Kwanini hawaridhiki namajukwa yao?
 
Soma biblia yako vzr, kwasasa hatuna cha madhabau waala kuhani,

Madhabahu ni mahali ambapo sadaka zinatolewa.. Katika Agano la Kale, Bwana Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wamtolee sadaka…Zilikuwepo sadaka za aina mbali mbali kama vile sadaka za dhambi, sadaka za shukrani na nyinginezo.

Lakini sadaka yoyote iliyokuwa inatolewa kama ni sadaka kuteketezwa, Ilikuwa ni lazima madhabahu itengenezwe. Kwa lugha rahisi na ambayo inaweza kueleweka ni kwamba baada ya mnyama yule aliyewekwa tayari kwaajili ya sadaka kuchinjwa..aliwekwa juu ya kuni zilizopangwa vizuri zilizo juu ya mawe…hivyo madhabahu ilitengenezwa kwa mawe na kuni..Ni sehemu maalumu ya kumchomea yule mnyama mpaka eteketee kabisa..

TUNA KUHANI MMOJA YESU KRISTO, NA HATUNA MADHABAU BALI TUNA VIBWETA VYA KUTOLEA MAHUBIRI
 
Soma: Waebrania 13:8
Daniel 7:25
 
Mtu yoyote anayesoma matangazo anaruhusiwa kutumia mimbari...

Kwetu sisi wakatoliki Sehemu ambazo huwezi kukuta mtu akisogea ni kule inakokaa ekaristi....pia ile meza ya padre ( vina majina yake)
 
Kanisani hakunaga cha Rais wala Makamu wala Waziri mkuu. Wote tunagombania kwenda mbinguni.

Vyeo hivyo vitabakia hapa duniani, kuingia mbinguni tunaingia kwa kumtumikia Manga, na kuwanyenyekevu, kwenda madhabuuni kufundisha wengine habari za Mungu.
Mtoa mada huna uelewa na mambo ya Mungu. pole sana
 
Tuwe wazi tu, huu utaratibu wameanzisha wakatoliki na wanaendelea kwa huyu VP nae amerithi huo utaratibu wa kutoa hotuba, nashauri TEC watoe maelekezo kanisa lisitumike kama sehemu ya kuendeleza propaganda za kisiasa.

Anayekuja kanisani aheshimiwe tu ila akimaliza asepe zake.

Nyerere miaka yote alikuwa anasali pale at. Peter's haya mambo hayakuwepo hata mzee Mkapa hakufanya haya, so as Mwinyi na JK kule misikitini unless iwe no kongamano la kidini Ila sio ibada.
 
Sasa hivi mnaandika tu bila woga.....naona wiki mbili tatu hizi post zimeongezeka mno watu wanafunguka tu
 
Mtoa mada ana uchungu kweli na dhamira yake lakini kikatoliki altare imegawanyika ipo sehem ya matangazo Kama hayo ambapo watu tofautitofauti hupewa fursa ya kuongea mfano wahamasishaji kutoka taasis mbalimbali.

Kama ilivyo kwa redio Maria lakin pia wasomaji wa injili za juma husika kwa somo la Kwanza na la pili,,,lakin pia na nafas kwa viongozi Kama hao,,,,

Kwahivo haiwezi kuzuilika lakini ipo sehemu iliyotakatifu kabisa hata Rais hawezi kuweka mguu wake eneo lile la ekaristi takatifu.,,,,

Kwa ufupi mtoa mada utapata kuwaelewa vema Wakatoliki!
 
Soma biblia yako vzr, kwasasa hatuna cha madhabau waala kuhani,

Madhabahu ni mahali ambapo sadaka zinatolewa.. Katika Agano la Kale, Bwana Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wamtolee sadaka…Zilikuwepo sadaka za aina mbali mbali kama vile sadaka za dhambi, sadaka za shukrani na nyinginezo.

Lakini sadaka yoyote iliyokuwa inatolewa kama ni sadaka kuteketezwa, Ilikuwa ni lazima madhabahu itengenezwe. Kwa lugha rahisi na ambayo inaweza kueleweka ni kwamba baada ya mnyama yule aliyewekwa tayari kwaajili ya sadaka kuchinjwa..aliwekwa juu ya kuni zilizopangwa vizuri zilizo juu ya mawe…hivyo madhabahu ilitengenezwa kwa mawe na kuni..Ni sehemu maalumu ya kumchomea yule mnyama mpaka eteketee kabisa..

TUNA KUHANI MMOJA YESU KRISTO, NA HATUNA MADHABAU BALI TUNA VIBWETA VYA KUTOLEA MAHUBIRI
Asante kwa ufafanuzi. Naona mkuu amechanganya akidhani bado tuko kwenye Agano la Kale na kusahau kuwa tuko kwenye Agano Jipya ambapo sote tunaoamini tumefanywa kuwa Ukoo wa Makuhani kwa njia ya Imani katika Yesu Kristo.
 
Naunga mkono hoja 💯. Yaani tumefikia hatua kiongozi tena mkubwa kabisa wa serikali anasimama mbele kwenye mimbari ya dini anatangazia umma kuwa kiongozi aliyeko hoi tena taabani kuwa ni mzima na ana chapa kazi. Hii na dhihaka ya wazi kabisa kwa Mwenyezi Mungu, Hili naomba lipigwe stop mara moja kwaajili ya kuheshimu nyumba takatifu za Mungu.
Waziri Mkuu alisimama mbele ya msikiti wakati wa sala ya Ijumaa na kuutangazia umma kuwa mwendazake yuko ofisini anachapakazi kazi na hana desturi ya kuzurula Kariakoo na Magomeni!
 
Nadhani tatizo lipo kwa viongozi wa Dini wenyewe wanajipendekeza kwa Viongozi wa Serikali,Kama kiongozi akija Ibadani na akafanya Ibada na kuondoka shida nn?

Ni vizuri kila kitu kikichukua nafasi yake

Vipngozi wa Dini naona ndio shida kukaribisha Viongozi wa Siasa wasalimie waumini,Halafu upo Ibadani unawaambia waumini Kodi unataka,ghafula unapoteza kumbukumbu yote ya Mahubiri ya siku hiyo
 
Mtu yoyote anayesoma matangazo anaruhusiwa kutumia mimbari...

Kwetu sisi wakatoliki Sehemu ambazo huwezi kukuta mtu akisogea ni kule inakokaa ekaristi....pia ile meza ya padre ( vina majina yake)
Watajulia wap hao wap.umbavu
 
Erasto Mbembati

Wewe ndiyo umeandika jibu Rais kwa swali gumu la mtoa post.

Umimi na ukwetu utatufikisha kubaya.

kiongozi wa kiserikali anaona sifa kusalia katika nyumba yake ya bada na kama haitoshi anatumia kodi ya wengine wasio wa kidini yake kujimwambafai.

Viongozi wa dini nao ni hivyo hivyo ni fahari kumsalisha kiongozi wa kiserikali ili kuwalingishia makundi mengine ya dini.

Sijui wapagani tujiweke wapi hapa.
 
Naunga mkono hoja [emoji817].

Yaani tumefikia hatua kiongozi tena mkubwa kabisa wa serikali anasimama mbele kwenye mimbari ya dini anatangazia umma kuwa kiongozi aliyeko hoi tena taabani kuwa ni mzima na ana chapa kazi. Hii na dhihaka ya wazi kabisa kwa Mwenyezi Mungu.

Hili naomba lipigwe stop mara moja kwaajili ya kuheshimu nyumba takatifu za Mungu.
Hatuna dini tena mkuu
 
Back
Top Bottom