Viongozi wa dini waiweka Serikali pabaya kuhusu Katiba Mpya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

KWA UFUPI
Akizungumza jana ikiwa ni siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema viongozi wa dini walitoa matamko ya hasira na yasiyokuwa na tija walipowataka wananchi kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, (TEC),Askofu Severin Niwemugizi alisema kulazimisha Katiba ipite kama ilivyo ni udhaifu mkubwa kwa sababu ina upungufu mkubwa ambao hautaweza kurekebishwa baadaye.


Dar es Salaam. Viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu wameendelea kuiweka Serikali katika wakati mgumu baada ya kusema hawataiunga mkono Katiba Inayopendekezwa ikiwa matakwa yao hayatazingatiwa.

Akizungumza jana ikiwa ni siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema viongozi wa dini walitoa matamko ya hasira na yasiyokuwa na tija walipowataka wananchi kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, (TEC),Askofu Severin Niwemugizi alisema kulazimisha Katiba ipite kama ilivyo ni udhaifu mkubwa kwa sababu ina upungufu mkubwa ambao hautaweza kurekebishwa baadaye.

“Naikataa kwa asilimia 100. Kwa kifupi, Rais akubali kutokukubaliana na sisi.”

Wakati askofu huyo akisema hayo, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Simba amesema iwapo Serikali haitaitambua Mahakama ya Kadhi na makadhi, Waislamu wataususia mchakato wa upigaji wa kura ya maoni kupitisha Katiba Inayopendekezwa.

Askofu Niwemugizi

Akizungumzia kauli hiyo ya Rais Kikwete, Askofu Niwemugizi alisema msimamo wa Jukwaa la Wakristo wa kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa haukuwa wa hasira, bali uliangalia kwa mapana masilahi ya Taifa katika miaka 200 ijayo.

Alisema ni udhaifu mkubwa kulazimisha kuipitisha Katiba ikiwa na upungufu na kusisitiza kuwa inatakiwa kutengenezwa kwa ustadi kwa sababu inagusa maisha ya Watanzania.

“Anaposema tamko letu lilikuwa la hasira na kuwa tuwaache wananchi waamue wenyewe anakosea kwa sababu Serikali yenyewe tangu ilipoizindua ilikuwa inawahamasisha wananchi waipigie kura ya ndiyo.

“Rais anaposema tusiwaamulie wananchi anakosea kwani hata sisi ni wananchi, lakini pia kutokana na nafasi zetu tunawawakilisha wananchi ambao hawana elimu, tuna wajibu wa kuwafundisha wasioelewa, wasiojua kusoma wala kuandika.”

Aliilaumu Serikali kwa kuipitisha Katiba hiyo mapema kabla haijaeleweka kwa wananchi.

Mufti anena

Mbali ya kutishia kususia mchakato wa kupitisha Katiba Inayopendekezwa, Sheikh Mkuu alisema Serikali haitatenda haki iwapo italiacha suala la Mahakama ya Kadhi mikononi mwa taasisi za kidini na kuitaka iitambue.
“Mbona CCM ililiweka hilo katika ilani ya uchaguzi mwaka 2010, halafu leo waseme kuwa wanatuachia wenyewe suala la Mahakama ya Kadhi? Hii si haki hata kidogo,” alisema Mufti Simba.

“Kama msimamo ndiyo huo basi sisi tutaendelea kuidai Mahakama ya Kadhi kama ambavyo tumekuwa tukisema siku zote na hatutaipigia kura hiyo katiba,” alisema alisema.

Kadhalika, alitaka Serikali kuacha kuliendesha suala la Mahakama ya Kadhi, ki- Bakwata Bakwata (Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania), bali ihusishe pia taasisi na jumuiya zote za Kiislamu ambazo zinawaunganisha Waislamu wote nchini.

Katika mkutano huo wa juzi, ulioandaliwa na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuwashirikisha wajumbe mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, Rais Kikwete alisema; “mwelekeo wa mambo hauhitaji uwe bingwa kujua hali hairidhishi, iwapo hatua hazitachukuliwa kutakuwa na uvunjifu wa amani wa kidini ambao moto wake ni mkali.” chanzo.Viongozi wa dini waiweka Serikali pabaya kuhusu Katiba Mpya - Kitaifa - mwananchi.co.tz

 
Wote wajinga sana tu kikubwa watu wapige kura kama haitapita tutumie katiba ya zamani hakuna cha zaidi tumechoka na ujinga wao wa kutaka wapigiwe magoti wakati watu wenyewe kwenye dini wamekaa kwa kificho tu wengi wauza madawa ya kulevya na biashara haramu kibao.
 
Katiba ya zamani ipo hatuna shida hata kidogo.
 
Hivi ni kwa nn viongozi wote wa dini ya kiislamu wana macho mekundu? Just curious
 
Mi nashangaa pia kwani tangu mwanzo ilisemwa katiba ikishindikana kupita,itatumika ya sasa,kwahiyo katiba sio hasa big ishu hapa.
kwani rais ajae ataleta katiba yake ready made itumike?si nae akitaka katiba atapitia process hizi hizi na kama itakwama,katiba ya sasa itapeta.
 
Hii katiba haitakiwi ipigiwe kura kipindi hiki cha uchaguzi yaani yatakiwa tusubiri uchaguzi uishe maana kwa sasa tutapata madudu sio katiba turekebishe tume ya uchaguzi mambo yaendeleee vinginevyo kazi ipoo udini utatumaliza
 
Yote haya ameyasababisha kikwete,sita, pinda na ccm yao kwa matumizi ya rushwa na udanganyifu ili kujimlikisha utawala wa nch ambayo ni ya Wtanzania.

Aliyewahadaa kuwapa mahakama si serikali bali ni ccm, hivyo wamalizane na ccm.

Lakini pia waislam waache kujidharaulisha kwamba hawana akili za kuelewa kwamba nchi hii inaongozwa kwa katiba. Katiba ya nchf hairuhusu serikali kufungamana na imani ya dini yoyote. Mbona hilo liko dhahiri? Kwa nini hawataki kukubali kwamba walidanganywa wakalichukua kama somo badala yake wanazidi kulazimisha tu kwamba udanganyifu huo uhalalishwe? Kweli wao ina maana hawajui umuhimu na uzuri wa kuheshimu katiba ya nchi?

Ina maana waislam hao, mtu akiwaambia wafanye naye biashara kwa ahadi kwamba atawapa mlima kilimanjaro na kuwamilikisha wizara ya fedha watakubali tu kwa kuwa wameahidiwa bila kujali uwezo na uhalali wa kutekelezeka kwa hiyo ahadi? Hawawezi kujua kwamba mlima Kilimanjaro haumilikiwi na mtu na kwamba hakuna mtu anaweza kuwapa wao wizara ya fedha? Kwa nini hawataki kuona kwamba ccm si mmililki wa katiba na hana uwezo wa kuvunja katiba na kuifanya atakavyo kwa kuwa katiba ni ya serikali na serikli ni ya watu wengine na si mali ya ccm?

Pamoja na kujua kwamba wamehadaiwa, kwa nini sasa wazidi kulazimisha Watanzania wenye katiba waivunje ili kutimiza ahadi laghai za ccm? Waislam ni watu wenye ufaham wao na akli. Sidani wanaweza kuwa watu wasioelewa kiasi hiki ch a kuendelea kulazimisha serikali itekeleze maagano yao haram na ccm.

Hakuna dini iliyoiweka mahala pabaya serikali. Serikali kwa tamaa ya ccm ndiyo imeiweka pabaya serikali kwa kujiingiza katika masuala ya dini zlizokuwa zimetuliwa zikiheshimu katiba ya nchi.

Dawa pekee si kuendeleza unafiki na kujenga nyufa na mitafaruku inayopelekea machafuko makubwa nchini. Serikali irudi kwenye nafasi yake ya kusimamia na kulinda katiba ya nchi!.

Kinyume cha pale, hakuna amani kwa kuendesha nchi kinafiki huku mkivuruga na kutengeneza machafuko kwa mikono yenu. NJE YA KATIBA HAKUNA MAELEWANO.
 
Ngoja kura zije tuwaonyeshe maajabu hawa viongozi wa dini sisi sio mapoyoyo. Kukataa au kukubali ni juu yetu wao haiwahusu kabisa wao zakwao sadaka mbona hawtuwaingilia kataka hilo la sadaka
 


 
 
 
ngoja kura zije tuwaonyeshe maajabu hawa viongozi wa dini sisi sio mapoyoyo. Kukataa au kukubali ni juu yetu wao haiwahusu kabisa wao zakwao sadaka mbona hawtuwaingilia kataka hilo la sadaka


ha ha ha ha kwa hili kura ya ndiyo kwa katiba mpya haiepukiki.
 


heleweki sijui unatoa hoja ,unajijibu mwenyewe au unatoa maoni yako au mapendekezo tuliza akili tukuelewe.
 
 
Tunalala sana kwenye misiba!!!
Wajameni tunapojibizana kwa hoja tuwe na busara na kiac, si vema kukashifu viongozi wa dini, pili tunafahamu ya kuwa serikali yetu haina dini that means it is a secular state, tunawahadaa hawa viongozi wanapozidi kuweka mashinikizo juu ya katiba hii, wajameni akili za kuambiwa changanya na zako, sote tuungane kwa pamoja tukapige kura ya ndiyo na kama mnakumbuka leo ndo kampeni kuanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…