#COVID19 Viongozi wa dini wakubali kufata maelekezo ya Wataalamu wa Afya katika kukabiliana na Covid-19

#COVID19 Viongozi wa dini wakubali kufata maelekezo ya Wataalamu wa Afya katika kukabiliana na Covid-19

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Viongozi wa umoja wa dini mbalimbali umesema msimamo wao katika mapambano ya ugonjwa wa Covid-19 ni kusikiliza sauti za wataalamu na wanasayansi ikiwemo maamuzi ya chanjo ya kupambana na ugonjwa huo.

Kauli ya viongozi hao imekuja siku chache baada ya chanjo zaidi ya milioni 1 za Covid - 19 kuwasili nchini, huku Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuzindua chanjo hiyo kesho kwa kuchanjwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Julai 27, 2021 Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Amani, Mwashamu Askofu Nelson Kisare wakati akizindua mjadala wa nafasi ya taasisi za dini na wadau juu ya elimu ya umma katika tokomeza Covid-19.

“Msimamo viongozi wa dini ni kuikubali chanjo na kwanini tunakubali chanjo? Kwa sababu Rais aliunda timu maalum ya wanasayansi kumshauri na kufanya uchunguzi njia ipi itatufaa.

“Mungu amesema watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa na katika hili maarifa ni chanjo. Katika hili chanjo ipi? Tumekubaliana tusikilize sauti za wataalamu kuna vyombo vimetumwa kufanya tafiti na kutoa taarifa sahihi watakaosikia kwa hiyari yao wanaweza kuchanjwa,” amesema Askofu Kisare.

Amesisitiza kuwa viongozi wa dini zote wameafiki kuwa wanataka kusikiliza sauti ya wataalamu, “wanasemaje tutasikia watakaposhauri baada ya kufanya tafiti mbalimbali na tutawashauri watu watumie chanjo ambazo ni sahihi.”
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Hamis Makata amesema,

“Viongozi wa dini tumekubaliana kufuata miongozo ya Wizara ya Afya, kuitekeleza kwa vitendo iliwemo kuhimiza waumini kunawakwa maji tiririka na sabuni, vipima joto na kikubwa tunataka kulinda uhai wa watu wetu na chanjo ni muhimu.”

Mwananchi
 
Corona inatafutwa kwa tochi Tanzania.

Tangazeni na lockdown kabisa ili mfanane na dunia inavyoenda.
 
Dini inadharaulika Sana siku hizi,,,kuna Ma-Askofu wa Katiba ,maAskofu wa Chanjo,,hadi maAskofu wa kuombea mikutano ya NEC sisiemu pale Dodoma...
 
Ndo maana simshangai mtu akinambia hataki maswala ya hizi dini make ni upuuzi na vyombo vya kuilainisha brain ya mwanadamu ili wafikie malengo yao binafsi
 
Back
Top Bottom