mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
Trend inaonyesha licha ya kuwepo maagizo ya kidini kusambaza imani zao. Bado wanasiasa wa ulaya watafuta Mali wakiarabu waliwatangulia wana dini kusambaa duniani. Yaani walianza wapererezi wamisionary nao wakafuata. Wengi walijikuta wanasambaza dini kisiasa.
Wanasiasa walipoanza kuhimiza Elimu dunia kama kigezo cha kupata cheo kikubwa. Watu walianza kusoma Degree, PHD, Masters. Bila kujua watu wa dini nao wakafuata mkumbo wakaanza na hadi sasa wanapigana vikumbo katk vyuo wakitafuta hadhi za Elimu Dunia. Cheo kikubwa kidini hupimwa kwa kiwango cha Elimu dunia ya muhusika huku viongozi waasisi wa imani hawakumaliza hata STD 7. Hizi ideas walizitoa kwenye siasa.
Wanasiasa walipogeukia Ujasiliamali na kuwekeza ili kuleta maendeleo. Bibilia na misahafu nayo ilihafifishwa na msisitizo ukahamia huko ambao wana siasa wanasisitiza. Nimehudhuria Mkutano mmoja wa Imani. Mtoa neno alipofikia hatua ya kusisitiza kazi, alipaza sauti, akakomaa kuliko alipokuwa anasisitiza lengo kuu la neno lake. Cha ajabu kesho yake hadi magazeti ya kidini yaliandika huo msisitizo wa kazi kwa sababu ndio msisitizo wa wanasiasa awamu hii.
Kila dini inamalengo yake, inakauli mbiu zake na kusudi. Nawapa ushauri viongozi wa kidini rudini katika mizizi Yenu kwa mini mpo. Msisitizo ya wana siasa waachieni wanasiasa. Mmeifanya dini kuwa kitu chepesi ndio maana Wasanii, wanamichezo na wanasiasa wanatamani nao madhabahu na mimbari maana hata wao wanaona ni kazi rahisi.
Nimeanza kuwa makini hata na maombezi ya viongozi wa kidini katika vipindi hivi vya kampeni. Ikiwa makini unaweza kuokota vipisi vya sentensi za kisiasa katikati ya maombi hayo. Unaweza ukaona kampeni katikati ya maombi hayo. Unaweza kugundua kiongozi haongei na Mungu Bali anawapanga wasikizaji wa maombi hayo ili wamuamini mwanasiàsa anayegombea kama wanavyomuamini yeye.
Mwisho: Bibilia inatutaka tufanye dua na Sala kwa wafalme na wakuu ili kuwe na haki na Amani ktk nchi. (1timotheo 2:1-4). Msizidi hapo mkaanza kupamba watu au kuoshabongo za waumini ili wamuamini mtu fulani.