Asalaam Aleykum,
Mwanzo 27:1-46, Biblia inaelezea kisa cha mzaliwa wa kwanza wa Mzee Isaka (Isihaka) ambaye aliitwa Esau pamoja na mdogo wake Yakobo (Yakub).
Kulingana na mila na tamaduni za kipindi hicho, Esau alikuwa ni kiongozi automatically kwa maana ndiye alikuwa mzaliwa wa kwanza.
Kwa bahati mbaya sana kufupisha hiki kisa ni kwamba, Esau alijikuta ameuza uzaliwa wake wa kwanza (ambao uliambatana na majukumu ya kiuongozi) kwa mdogo wake (Yakobo) kutokana na njaa kali aliyokuwa nayo siku moja, kwa bakuli la kunde!
Ijapokuwa hiki kitendo kilifanyika kwa muda mfupi sana, lakini kilikuja kubadilisha kabisa hatma ya maisha ya Esau na uzao wake milele.
Biblia katika kitabu cha Waebrania 12:16,17 inaeleza kwamba Esau alikuja kujutia sana baadaye tena kwa machozi, lakini hakuweza tena kupata kile alichokipoteza kwa mlo mmoja tu.
Hivyo ndivyo walivyo viongozi wengi wa nchi za Kiafrika. Wako tayari kuuza au kumilikisha maliasili zenye rhamani kubwa sana kwa maslahi ya muda mfupi sana.
Hili hata halihitaji ufafanuzi kwa maana sote tunajua kile ambacho viongozi wa Kiafrika wamekuwa wanatoa in exchange of kondomu, kujengewa matundu ya vyoo, kujengewa madarasa, n.k.
Mungu awasaidie sana viongozi wa Kiafrika ili waweze kusahihisha makosa ambayo wamekuwa wakiyatenda kwa siku nyingi kama ambavyo Esau aliomba babaye ambariki walau kidogo.
Kwa sababu makosa yalishafanyika huko nyuma, hatuwezi kuendelea kukosea ilhali nafasi ya kujirekebisha ipo. Ukigundua umekosea njia, haina haja ya kuendelea mbele hata kama umeshatembea umbali mrefu, unatakiwa ugeuke nyuma na kurudi hadi pale ulipokosea, kisha uendelee na safari yako kwa njia sahihi.
Nawatakia wakati mwema.