Viongozi wa Kiroho lipeni kodi kwa wakati ili kuepuka fedheha katika jamii

Viongozi wa Kiroho lipeni kodi kwa wakati ili kuepuka fedheha katika jamii

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Hapa nina wazungumzia Wachungaji, Masheikh, Mapadre na wote ambao ni viongozi wa kiroho, heshima yenu ni kubwa mno katika jamii na mnategemewa kuwa mfano mbora katika jamii yetu. Siyo wote ambao mna nyumba zenu binafsi, hivyo kuwalazimu kupanga na kujistiri katika nyumba hizi na kufanya makazi yenu.

Nakutana na kisa kimoja ambacho mpaka kimenifanya niandike uzi huu, ili hizi aibu ndogo ndogo muweze kuziepuka kwa kulipa kodi za watu ndani ya muda husika mkichukulia nyie ni watu muhimu sana.

Nafungua code kama ifuatavyo;

Nipo zangu njiani kwa mbali kidogo nawaona wamama wawili wanakuja huku wanaongea mambo yao, nami napiga hatua zangu mdogo mdogo, nilipo karibiana nao kama tunapishana hivi ndiyo nikajua wanazungumzia nini kwasababu walikuwa wanaongea kwa sauti kubwa kiasi!

"Mchungaji anadaiwa kodi na bado hajalipa,hivi kwani sadaka zao huwa wanafanyiaga nini?"

Nilibahatika kumsikia msemaji mmoja na hao wakanipita, hiyo kauli moja kwa wale waliopitia mafaili ya Cuba ilitosha kujua hapa kuna mtumishi wa Mungu anadaiwa kodi ya pango na hajalipa.

Kudaiwa kodi siyo jambo la ajabu wala la kushangaza, lakini swali linakuja inakuwaje mpaka majirani wajue kuwa kiongozi huyu wa kiroho anadaiwa kodi? Ina maana hakuna usiri kati ya mpangaji na mwenye nyumba mpaka inapelekea wapangaji wengine kujua hali ya huyu bwana mkubwa.

Nini kifanyike?

Viongozi wa kiroho ili kulinda heshima yenu katika jamii basi mjitahidi kulipa kodi zenu kwa wakati ili muepuke hizi fedhea kutokana na hadhi zenu katika jamii. Ebu fikiria ni wangapi mtaani kwako watajua kuwa wewe siyo mlipaji mzuri wa kodi?

Lakini Etugruel Bey akichelewa kulipa kodi siyo habari wala siyo ishu kwakuwa sina wadhifa wowote mkubwa lakini nyinyi ni lazima iwe ishu kama nilivyodaka maongezi ya wale wamama.

Wenye nyumba nanyi, pamoja na kwamba mna haki ya kudai kodi zenu lakini basi mjitahidi kuwastiri hawa viongozi wetu. Je, kuna haja gani mpaka wapangaji au watu wengine wajue Mchungaji au Sheikh anadaiwa kodi ya nyumba? Nawaomba muwape heshima yao wanayo stahili na Mungu atawabariki sana.

Nawapenda sana viongozi wa kiroho kwasababu nyinyi ndiyo mnaifanya jamii iwe katika mstari.

Ni hayo tu!
 
Nilidhani unashauri sadaka ikatwe kodi, hilo ndo la msingi.
 
Hivi unaitwa Etugre bey au Etugre boy?
 
Nilidhani unashauri sadaka ikatwe kodi, hilo ndo la msingi.
Hilo ulilosema ni katika ngazi ya Kanisa au msikiti lkn hapa nazungumzia kiongozi kama kiongozi katika swala zima la kulipia makazi yake.

Lakini

Sio makanisa na misikiti yote ambayo inauwezo WA kukusanya sadaka ambayo unaweza sema ikaweza kulipiwa Kodi

Hili nalo mliangalie
 
Back
Top Bottom