Moja ya Amri za Mungu katika kitabu cha kutoka 20 ni kuikumbuka siku ya Sabato na kuitakasa.
Na hakuna ubishi kuwa siku ya saba ndiyo siku ya Sabato. Pia hakuna ubishi kuwa siku ya saba ya juma ni jumamosi. Labda kwa waswahili tu ambao wengi ni wavivu wa kusoma na kufikiri.
Hata hivyo ninasikitika kwa viongozi wa dini kujuzima data na kuendelea kuhukumu watu kwa vitu vinavyoweza kufafanuliwa vikaeleweka lakini wao wamechagua kuwa mafarisayo.
Nitawafanya mjiulize maswali kisha myajibu ama mbaki kuwa hivyo mlivyo kama vikwazo vya roho zinazotamani kupata majibu sahihi.
1. Kanisa la SDA( wasabato) mnamiliki hospitali.Je hamfanyi kazi siku ya Sabato?
2. Je mnakubali ili hospitali ifanye kazi vizuri lazima kuwe na umeme?( Tanesco wawe kazini)
Kwamba wagonjwa wengine watakuja kwa usafiri wa umma ( kwamba boda boda,tax na daladala wawe kazini?)
3. Je makanisa,ofisi zenu na majengo yenu yana walinzi wanafanya kazi siku saba kwa wiki ikiwepo na siku ya Sabato?
4. Je mtu kuna sehemu yoyote kwenye biblia inaonesha utaratibu wa ibada inayofanyika siku hizi kwamba usipoifaya hiyo ndio unaonekana hujashika Sabato?
Iwapo mtu ataishi maisha ya utakatifu,bila kufuata mipangilio yenu ya ibada bado ni mvunja Sabato au mvunja kanuni za kanisa la kisabato?
5. Mnazungumziaje kauli ya "msiisumbukie kesho" aliyosema Yesu mwenyewe,pia katika kitabu cha Waebrania kinapozungumzia Sabato, kinasema wazi Mungu alitoa siku nyingine.Hiyo siku nyingine akailezea ni ipi.
Alinukuu Daudi akiisema hiyo siku nyingi kuwa ni "Leo"
Mwanadamu amepewa siku moja tu iitwayo " Leo" .Kwamba kila iitwapo leo binadamu anapaswa kuwa mtakatifu kwa kuisikia sauti ya Bwana.Je mtu aishiye "Leo" ..kwa kumtukuza Mungu,anawezaje kuvunja Sabato ya siku ya Saba?
Mwisho niwatakie Sabato njema na kila mmoja kuitafakari kila leo Mungu anayompatia