Jibu lake ni simple tu, Je ikiwa ng'ombe wako atatumbukia kisimani utamuacha kumtoa kisa ni siku ya sabato ? Sidhani, basi ni halali kutenda mema siku ya sabato.
Kitu cha ziada, dunia imebadilika kiasi kwamba watu wametofautisha vingi na vyote vinachukuliwa kama kazi
Ilhali kiuhalisia na kitafsiri ya kiimani ni kama ibada, kitu kama kutoa msaada, kutibu mgonjwa, kuuguza n.k
Kuiheshimu Sabato kunaanza na kuweka umuhimu wa kutofanya kazi na kuitumia kwa ibada na pumziko
Mfano. Nauza Duka la vifaa vya ujenzi or stationery, electronics hivi vitu nikifunga siku ya sabato kuna kosa gani?? Sababu ni kazi kama kazi nyingine na hakuna udharura wa hiko
Kuhusu hospitali hiyo ni dharura na ni muhimu kuwepo wakati wote,
Je kuna mtu ataenda hospitali ikiwa si mgonjwa?
je ushawahi kwenda hospitali muda wa usiku??
Je ulikuta watu 100?? Unakuta mtu wa zamu (nesi/daktari) lakini utapata matibabu na hiyo ndio dharura ambayo utaiona kazi ila kiimani ni ibada
Hospitali itakuwa wazi kwa dharura na sio full operational kama ilivyo siku nyingine zote kutoa fursa kwa wafanyakazi wote kupata pumziko kama ilivyo msingi wa sabato ya kweli na ya Bwana