Katika ibaada hiyo Mwenyekiti wa Chadema Taifa Tundu Lissu aliwaongoza waombolezaji katika safari ya Mwisho ya Magoma hapa Dunia.
Mh. Lema, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, aliongeza: "Dr. Mollel, tunakushukuru sana. Hata wakati tunamsafirisha Magoma nje ya nchi, ulikuwa msaada mkubwa." Huu ulikuwa ni uthibitisho wa juhudi za pamoja za viongozi.
Katika salamu zake, Dr. Mollel alisisitiza umuhimu wa afya na ustawi wa jamii. "Niwapongeza sana viongozi wote wa CHADEMA, wakiongozwa na kaka yangu Golugwa na Mh. Mbowe, kwa juhudi zenu za kuyapigania maisha ya Magoma. Magoma ameacha watoto, naomba niwalipie ada Tsh milioni nne. Na kama hutojali, shemiji yangu, niruhusu niwasomeshe watoto wa Magoma." Wananchi walijibu kwa shangwe, wakipiga makofi, kitendo kilichopelekea kukubaliwa kwa ombi hilo.
Dr. Mollel alikumbusha wananchi kupima afya zao mara kwa mara, akisema Rais Dr. Samia ameleta vifaa vya kisasa katika hospitali zetu. Alisisitiza umuhimu wa kuzingatia masuala ya lishe na mazoezi, akieleza: "Dr. Samia amekuwa jemedari wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya. Amewekeza katika vifaa vya kisasa nchini. Ebu jiulize, leo tuna vifaa ambavyo, ikiwa mtu ana uvimbe kwenye sakafu ya ubongo, tulikuwa tunafunuwa fuvu lote. Ila leo, Dr. Samia ameleta vifaa ambavyo, ndugu yangu Lema, ukiwa na shida hiyo, tunaweka kifaa kwenye pua hapo na tunaondoa uvimbe huo."
Aliongeza: "Pia, leo kaka yangu Lissu, ukiwa na shida ya moyo, hatufanyi operesheni zile za zamani. Tunakutoboa sentimita mbili tu na kutibu tatizo la moyo,huna haja ya kwenda Canada tena, hizi huduma zinafanyika hapa nchini. Na Dr. Samia ameiweka nchini na watu kutoka nje ya nchi yetu wanakuja kwa sababu tuna vifaa vya kisasa na bei ni nafuu mno. Hii ni kazi ya jemedari wetu, Rais wetu Dr. Samia na hapo Dr Samia amewekeza Tsh 6.5Trilioni kwenye vifaa nchini."
Katika hatua nyingine, Dr. Mollel alisema kuwa watashirikina Kwa pamoja na viongozi wa CCM na Serikali kuhakisha wanakamilisha kiasi cha Shilingi Million Kumi na tano ili kuendeleza ujenzi wa msikiti wa Magugu Matufe. Shehe wa eneo hilo, ndugu Kesi, alitoa shukrani akisema: "Tunakushuru sana, tupelekee salamu zetu serikalini, na tunawaombea."
Maziko ya Derick Magoma yamekuwa ni tukio la kuwakumbusha wengi kuhusu umuhimu wa umoja na msaada katika kipindi cha majaribu. Dr. Magoma amezikwa katika kijiji chake cha Magugu akiwa na umri wa miaka 40, na ameacha mke na watoto watatu. Hali hiyo ilionyesha kuwa, licha ya huzuni, kuna matumaini ya kuendelea kusaidiana na kujenga jamii imara.