Viongozi wa Kkidini wamepotoka rudini kwenye mstari

Viongozi wa Kkidini wamepotoka rudini kwenye mstari

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Matatizo mengi yanaendelea kuzikikumba jamii na familia katika kipindi hichi cha kidigital,maadili kuharibika uhuni na umalaya kuongezeka jamii imeoza kwa tabia chafu na mitazamo hafifu ya binadamu.

Katika maisha zipo taasisi ambazo zinazo simamia maadili ya kila mmoja wetu kwa kuweza kurekebisha tabia na mienendo mibaya ya wanajamii mfano taasisi za kidini,jeshi la polisi na viongozi wa utamaduni lakini kwa bahati mbaya vyombo vingi venye kusimamia haya maadili navyo vimecorrupt kimbinu na mitazamo katika utekelezaji wake.

leo nitaongeleza zaidi taasisi na viongozi wa kidini kwa kuonyesha jinsi gani wameshindwa kutekeleza majumu yao na baadala yake wanatumia majukwaa haya kwa kuharibu tamaduni au maadili .

CHANGAMOTO KATIKA JAMII
kila tatizo hutatuliwa kwa kuweza kuukabili au kiini cha tatizo hilo jamii imeharibika na ndoa kuvunjika masheikh au wachungaji ndiyo watu sahihi kulitatua tatizo ndio kwanza wanaharibu au wanalijibu tatizo hili kwa kutibu juu juu.

KUVUNJIKA KWA NDOA
unawezaa kukuta kiongozi anatokwa jasho kutafuta umaarufu kwa kuyiongelea ndoa kwa waumini kumbe tatizo sio ndoa ila maadili ndio yamecorrupt na maadili yanahiribika kwa uwepo wa mitandao hivyo na kupelekea ndoa nyingi kuvunjika,sasa njia ya kulitibu tatizo hili ni kurejesha umma katika kumuamini mungu na kuwashawishi watu wamrudie muumba pamoja na maamrisho wake lakini utamkuta mtu kashupaa kwenye mada ya ndoa lengo ni kuvutia watu ili ajulikane na kupata fedha za kumuendeshea maisha yake.

WIZI NA UMALAYA
wakumbushaji wengi hawaongelei kuwa mzizi wa tatizo kuwa ni malezi mabaya ya watoto baadala yake wanabased kwenye impact ya tatizo sasa hapa tunajenga na kuizidisha jamii kuendelea na kulipalilia tatizo hili kwa kiasi kikubwa.

HITIMISHO
nimeleta mda hii ili tuweze kujadili misingi sahihi ya kuisaidia jamii kuondokana na tatizo la upotefu wa maadili na kuwakumbusha wakushaji namna nzuri ya kuirejesha jamii kwenye mstari ila ningependa kwanza kabla ya hawa wakumbushaji hawajaleta mada kwa jamii husika wanapaswa kufikiria mada wanayoleta na maneno wanayoropoka yataleta athari gani
 
Jamii Bora na Salama huanzia katika Familia zetu. Ugumu wa maisha unatupa wazazi wakati mgumu wa malezi, mzazi anaondoka nyumbani saa 11 alfajiri anarudi saa sita usiku.

Anaondoka watoto wamelala anarudi watoto wamelala.

Changamoto kubwa inaanzia matika malezi kwa ngazi ya familia.
 
Yameshatabiliwa haya hayana budi kutokea cha msingi linda imani yako.

Kadri makanisa na misikiti inavyoongezeka ndivyo maovu nayo yanaongezeka.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom