Haiingii akilini kuona viongozi Wa klabu kama simba kufanya udanganyifu Wa mikataba Na kushindwa kuitekeleza kisha kukimbilia kuzilaumu mamlaka kuwa zinawahujumu.wakati dunia nzima vilabu vinatafuta wachezaji wenye umri mdogo viongozi Wa klabu ya simba inampoteza mchezaji Ramadhani singano kwa ubabaishaji Wa kitoto unaofanywa Na hao viongozi.Hongera Azam kwa kumsajili mchezaji huyo na ninatoa wito kwa wachezaji vijana ndani ya simba kuamka Na kutafuta vilabu vingine ili mpate maslahi Mpira ni Pesa sio longolongo za viongozi Wa simba
Kama inshu ni maslahi, Simba SC imewaongezea wachezaji wake wafuatao mikataba.
- Jonas Mkude. Kalamba 70m, GX 110, mshahara 2m kila mwezi na mkataba miaka miwili.
-Said Ndemla. Kalamba 35m, mkataba miaka miwili.
-Hasssan Isihaka. Kalamba 35m, mkataba miaka miwili.
-Abdi Banda. Kalamba 20m, Analiapiwa Jodi ya nyumba, mkataba miaka miwili.
Walio katika mazungumzo ya kujazwa minoti: Manyika Jr na Awadh Juma a.k.a Mtani Jembe.
Sasa Mkuu ni timu gani nyingine ukiacha hizi 2 za dar zinaweza kuwalipa hivi wachezaji makinda?! Na ndo maana tunaishia kuwaona kina Kaseke, Mwashiuya, Mwalyanzi, Emanuel Ntinde wakija mjini.
Hawa madogo wanatakiwa wakaze sana, kwani mambo mazuri yanakuja.