Viongozi Wa klabu ya Simba hawafai

Viongozi Wa klabu ya Simba hawafai

mhakikimali

Member
Joined
Jul 5, 2015
Posts
31
Reaction score
5
Haiingii akilini kuona viongozi Wa klabu kama simba kufanya udanganyifu Wa mikataba Na kushindwa kuitekeleza kisha kukimbilia kuzilaumu mamlaka kuwa zinawahujumu.

Wakati dunia nzima vilabu vinatafuta wachezaji wenye umri mdogo viongozi Wa klabu ya simba inampoteza mchezaji Ramadhani singano kwa ubabaishaji Wa kitoto unaofanywa Na hao viongozi.

Hongera Azam kwa kumsajili mchezaji huyo na ninatoa wito kwa wachezaji vijana ndani ya Simba kuamka Na kutafuta vilabu vingine ili mpate maslahi Mpira ni Pesa sio longolongo za viongozi Wa simba
 
Nasubiri tamko la Manara. Hivi hawa viongozi wanawaona mashabiki wote wa mikia ni mambumbumbu eeeh
 
Sio Simba tu, ni Pamoja na Yanga na vilabu vingine. Tatizo ni siasa katika michezo. Zile kauli za kilimo ni siasa, michezo ni siasa ndizo zinazotogharimu. Mtindo huu wa kupoteza Yoso kama Singano na Ndemla kwenye vilabu vikongwe ni ishara ya ubabaishaji katika uongozi wa vilabu. Nashauri Singano akafingue jalada ili pia tubaini uwepo wa mkataba tofauti kwenye timu ya simba na ule aliosaini yeye.
 
Yanga wamepoteza yoso gani tena? Na Ndemla naye anaondoka?
 
Nafikiri simba kuna tatizo la uongozi. Vijana wote zaidi ya 30 (ambao wanaweza kuunda timu nzima) waliokuzwa na matola na rage wakapigwa msasa na babu mfaransa liewig wameondoka kutokana na kutothaminiwa wamebaki kama 5 tu.

Mbaya zaidi wameondoka wakati wameshakomaa na wapo tayari kushindana katika ligi kuu. Leo kila mtu duniani anaisifu barcelona namna inavyocheza lakini siri kubwa ni kutegemea makocha waliokuwa wachezaji wao zamani na wachezaji vijana inaowakuza kila mwaka na usajili wao huwa wanaongeza wachezaji 1 - 2 supastaa ambaye anaendana na staili yao ya uchezaji.

Kwa wanaojua mpira simba ya mwaka jana ilikosa pumzi, stamina, kiungo mshambuliaji ambaye ni mbunifu na mshambuliaji wakati mwenye uwezo kama amisi tambwe basi lakini cha ajabu wamekimbilia kusajili wachezaji kwa mamilioni na kumpuuza singano kwa nini asiondoke?

Nenda singano nenda labda viongozi watajifunza kutokana na makosa waliyofanya.
 
Joo Wane inawezekana kweli kuna mistake ilifanyika hadi hapo graduate wa Simba B wakasepa, lakini nataka nikuume sikio kidogo. Si kila graduate wa academy anaweza qualify kucheza first eleven.

Hiyo Barca unayoizungumzia tangu lile darasa la kina Messi, Iniesta lifanikiwe kupenya 1st eleven, hakuna aliyeweza kupenya tena ukiacha busquet na Pedro wanaojaribu kuingia 1st eleven, japo kila mwaka kuna graduates wanafuzu kama vile el hadari, batra, rafinha..

Alafu hapo magraduate wa Simba B kama walikua wapo tayari kushindana kwa ligi kuu wako wapi Siku hizi??! Kama unajua uanajua tu.. Mbona hatuwaoni??
 
Last edited by a moderator:
Haiingii akilini kuona viongozi Wa klabu kama simba kufanya udanganyifu Wa mikataba Na kushindwa kuitekeleza kisha kukimbilia kuzilaumu mamlaka kuwa zinawahujumu.wakati dunia nzima vilabu vinatafuta wachezaji wenye umri mdogo viongozi Wa klabu ya simba inampoteza mchezaji Ramadhani singano kwa ubabaishaji Wa kitoto unaofanywa Na hao viongozi.Hongera Azam kwa kumsajili mchezaji huyo na ninatoa wito kwa wachezaji vijana ndani ya simba kuamka Na kutafuta vilabu vingine ili mpate maslahi Mpira ni Pesa sio longolongo za viongozi Wa simba

Kama inshu ni maslahi, Simba SC imewaongezea wachezaji wake wafuatao mikataba.

- Jonas Mkude. Kalamba 70m, GX 110, mshahara 2m kila mwezi na mkataba miaka miwili.

-Said Ndemla. Kalamba 35m, mkataba miaka miwili.

-Hasssan Isihaka. Kalamba 35m, mkataba miaka miwili.

-Abdi Banda. Kalamba 20m, Analiapiwa Jodi ya nyumba, mkataba miaka miwili.

Walio katika mazungumzo ya kujazwa minoti: Manyika Jr na Awadh Juma a.k.a Mtani Jembe.

Sasa Mkuu ni timu gani nyingine ukiacha hizi 2 za dar zinaweza kuwalipa hivi wachezaji makinda?! Na ndo maana tunaishia kuwaona kina Kaseke, Mwashiuya, Mwalyanzi, Emanuel Ntinde wakija mjini.

Hawa madogo wanatakiwa wakaze sana, kwani mambo mazuri yanakuja.
 
Nasubiri tamko la Manara. Hivi hawa viongozi wanawaona mashabiki wote wa mikia ni mambumbumbu eeeh

Manara kasema kwamba azam ndiyo iliyoihujumu simba kwa kuwa mpango wa kumsajili ulianza tangu zamani........"sisi tunatambua kama mchezaji wetu na hatujapewa barua rasmi ya kuvunjwa mkataba, yeye tayari kasaini, huu mpango waliuandaa tff na azam".
 
Mlimkataa Wambura mkamchagua Aveva kibaraka wa Hans Pope sasa mtajuta.Kuondoka kwa Okwi na Singano lazima kutakuwa na mkono wake,si anarudisha gharama zake bwana!
 
Mlimkataa Wambura mkamchagua Aveva kibaraka wa Hans Pope sasa mtajuta.Kuondoka kwa Okwi na Singano lazima kutakuwa na mkono wake,si anarudisha gharama zake bwana!

Singano kaondoka bure, kwakuwa TFF wamesema yuko huru.. Ila kuhusu Okwi ni hela nyingi timu imeingiza.
 
Singano kaondoka bure, kwakuwa TFF wamesema yuko huru.. Ila kuhusu Okwi ni hela nyingi timu imeingiza.

kwani okwi alisaini lini mkataba na simba baada ya kwisha ule wa miezi 6???
 
kwani okwi alisaini lini mkataba na simba baada ya kwisha ule wa miezi 6???

Kipindi cha dirisha Dogo la usajili, Okwi aliongeza mkataba wa mwaka mmoja, pia akaongezewa USD dola 1000 katika mshahara wake, na ndo mana akaendelea kuwatesa makipa mbali mbali katika ligi.
 
Sio viongozi tu hata wanachama waliwahi kuitwa mbumbumbu
 
Manara kasema kwamba azam ndiyo iliyoihujumu simba kwa kuwa mpango wa kumsajili ulianza tangu zamani........"sisi tunatambua kama mchezaji wetu na hatujapewa barua rasmi ya kuvunjwa mkataba, yeye tayari kasaini, huu mpango waliuandaa tff na azam".
kaishiwa mbinu huyo okwi wapi sasa hivi..
 
Back
Top Bottom