Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Wanajamvi, Leo naomba nilete kwenu giza hili la Tabora, kiukweli nimesikia mara kadhaa baadhi ya Viongozi wa Tabora kupiga kampeni ya kwamba, Tabora linatakiwa kuwa Jiji, kwa Giza hili hadhi ya jiji watapata wapi?
Viongozi wa Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora hili la Taa walichukue kama changamoto wahakikishe Taa zinawekwa na Mji unapendeza.
Taa za Barabarani ziko Ipuli pekee na baadhi ya maeneo ya Mjini lakini barabara ya kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ni Giza, Barabara ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete haina Taa.
Tunataka Mkoa ukue kimaendele, tuanze na vitu vidogo kama hivi ambavyo vinaonekana havina umuhimu, uwepo wa taa Barabarani unaweza saidia muonekano mzuri, unasaidia madereva na wapita njia, pia uwepo wa giza unaweza kuwa chanzo la kushawishi wahalifu kujificha kwenye maeneo hayo.