Viongozi wa masoko Dodoma Jiji wajengewa uwezo wa usimamizi masoko

Viongozi wa masoko Dodoma Jiji wajengewa uwezo wa usimamizi masoko

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
VIONGOZI WA MASOKO DODOMA JIJI WAJENGEWA UWEZO WA USIMAMIZI MASOKO

- Mbunge Mavunde awataka kusimamia huduma bora na utunzaji wa Mazingira.

- Kuwanunulia Kompyuta na Photocopier kwa ofisi za masoko yote.

- Rais Samia apongezwa kwa ujenzi na ukarabati wa masoko Jijini Dodoma

- Jiji la Dodoma lapongezwa kuandaa Mafunzo.

Viongozi wa masoko ya biashara ya Jijini Dodoma wamepata mafunzo ya siku tatu ya kujengewa uwezo juu ya usimamizi wa uendeshaji masoko na usimamizi wa biashara yaliyoandaliwa na Jiji la Dodoma kwa ushirikiano na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.

Akifungua mafunzo hayo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewataka viongozi hao kutumia elimu watakayopata kuongoza na kusimamia masoko Jijini Dodoma kwa uweledi mkubwa ili kusaidia kuboresha huduma kwa wateja na kuwaratibu vizuri wafanyabiashara hao.

Aidha Mbunge Mavunde alisisitiza juu ya usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya biashara na kuahidi kuwapatia viongozi hao wote vitendea kazi vya computer na photocopier katika ofisi zao ili kuboresha utoaji wa huduma.

Akizungumza katika Mafunzo hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Cde Charles Mamba amelipongeza Jiji la Dodoma kwa kuandaa mafunzo hayo kwa viongozi wa masoko na kutaka kufanyika kwa mafunzo ya aina hii mara kwa mara ili kuwajengea uwezo viongozi.

Naye Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Mh. Jabir M. Shekimwei amesema kwamba serikali inaendelea na zoezi ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa masoko mapya kwa lengo la kusogeza huduma kwa Wanadodoma na kuchukua fursa hiyo kumpongeza Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi mkubwa wa TACTIC ambao umelenga kuboeresho miundombinu ya barabara na masoko Jijini Dodoma.

IMG-20240530-WA0038.jpg

IMG-20240530-WA0037.jpg

IMG-20240530-WA0039.jpg
 
"Kuwanunulia Kompyuta na Photocopier kwa ofisi za masoko yote."

👆

Ninavyofahamu mimi, kwa mujibu wa sheria, masoko huanzishwa, kumilikiwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Halmashauri kupitia wataalam wake.

Nilitarajia hii elimu ingeelekezwa kwa wataalam wa Jiji na siyo hao wawakilishi wa wafanyabiashara.

Mfanyabiashara haendeshi soko, bali viongozi wao ni wawakilishi tu wa wafanyabishara kwenye vikao kati ya Halmashauri na wafanyabishara.
 
Back
Top Bottom