KERO Viongozi wa Mkoa wa Iringa na Wilaya ya Mufindi wanatupuuza Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mafinga, Rais Samia tusaidie

KERO Viongozi wa Mkoa wa Iringa na Wilaya ya Mufindi wanatupuuza Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mafinga, Rais Samia tusaidie

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wafanyabiashara wa Soko Kuu Mafinga tunaomba kufikisha kero yetu kwa Mamlaka za Juu akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Fedha na Rais Samia na kero hiyo ni kupuuzwa kwa madai yetu kunakofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi

Kwa takriban mwaka sasa tumekuwa na majadiliano yasiyofika mwisho na kila tukihitaji kupata mwafaka wa jinsi ya uendeshaji wa Vibanda ambayo tulikuwa tunavimiliki mwanzoni lakini baadaye serikali ikasema vipo katika eneo ambalo halijapimwa na hivyo itavichukua rasmi tofautiu na hapo tuanze kulipa kodi ya pango kwa halmshauri. Hilo si tatizo kwetu, tuko tayari kulipa lakini si kwa kiwango ambacho Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Serukamba imetulazimisha tulipe na tukikataa anakuja na Magreda kubomoa vibanda.

Pia soma: Mafinga: Mgomo wa Wafanyabiashara waingia siku ya 4, RC Serukamba asema yeye hana majibu waulizwe waliogoma

Hali hii inatumiiza sana wafanyabiashara wa eneo hili na kila tukihitaji kuzungumza naye anatutisha na kutupuuza. Sisi tuko tayari kulipa Kodi ya Serikali lakini kwa gharama ya Tsh. 50,000 kwa mwezi na si 80,000 kwasababu biashara si nzuri kiasi ambacho tunaweza kulipa fedha hizo.

Lakini kubwa zaidi ni kuwa hawa viongozi wanatunyanyasa sana ndiomana tumefikia hatua ya kufanya Mgomo kwa zaidi ya siku 4 sasa ili watusikilize shida zetu lakinu Serukamba anasema yeye hana majibu na hajui kwanini tunagoma. Sasa kiongozi wa aina gani anaweza kutoa kauli hizo dhidi ya Watu wake?

Rais Samia tafadhali tusikilize wewe, hawa viongozi unaotuletea hawatufai.
 
Back
Top Bottom