Viongozi wa Pamba walitangaza rasmi kujiweka pembeni siku walipocheza na Yanga pale Chamazi na kulambwa mabao 3 - 0 leo sishangai yanayotokea Mwanza

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Hakuna ubishi kuwa baadhi ya viongozi wa Pamba ni wanachama wa Yanga na walitangaza dhahiri kwenye mitandao ya kijamii wakati walipocheza na Yanga na kutafunwa mabao 3 0 kuwa baadhi yao wanajiweka kando kwa sababu wana maslahi na Yanga, watarudi kwenye uongozi baada ya mchezo huo.

Jambo hili nilililaani sana siku ile na niliandika humu humu Jamiiforums kuwaponda viongozi makanjanja kama hao.

Leo huko Mwanza mnyama kafanyiwa sana vurugu ili wale viongozi waliotangaza maslahi yao Yanga wakati ule wawafurahishe watu wa jangwani.

Pamba ya kuizuia Simba kesho iko wapi? Minziro huyu huyu kanjanja aizuie Simba?

Simba na Pamba hawakuwa na mahusiano mabaya tangu miaka hiyo tunazijua hizi timu, leo watu wengi wa Mwanza waliovamia mpira wakiwemo viongozi ambao wana matumbo makubwa na mijezi yao ya Yanga.

Miaka ya 1990 Simba ilikuwa inasajili sana wachezaji wa Pamba kuliko timu yoyote ile, Yanga ilibahatika kumchukua beki wa kulia mkatili David Mwakalebela, Fumo Felician wakati Simba ilimbeba Deo Mkuki, Dan Mhoja, Alphonce Modest, George Masatu, Hussein Masha, Nteze John, Bitta John, marehemu Rajab Msoma, marehemu John Makelele nk.

Leo viongozi wa Pamba wenye unasaba na kujipendekeza kwa Yang wanaifanyia fujo Simba ili kuwaondoa mchezoni kesho? Shame on you.

Pamba mmefukuza kocha, leo mmemuokota Minziro ndio mkamsumbue Ateba, Ahoua, mbona vituko hivi.

Acheni mambo ya kitoto, vurugu hizo ni dalili kuwa mnatumika na wala sio vinginevyo, mnautoa wapi upinzani na Simba nyie, mbona nyie na Simba ni mbingu na ardhi?
 
Ukiweza kuwazuia Simba wasifanye vitendo vya kishirikina kabla ya mechi lazima wataleta fujo.
 
Kwa hiyo Simba imesajili waganga wa jadi halafu pamba imesajili wacheza soka sio?
Ukipata jibu nenda chooni kafungue zipu ujikague jinsia yako maana unatia shaka
 
Wameshakula hela za mjinga wao Yanga hao wacha wahangaike.
 
Kama wanatakaka vita tuwasubirie waje dar tushughulike nao makumazani.
 
Hakuna ubishi kuwa baadhi ya viongozi wa Pamba ni wanachama wa Yanga na walitangaza dhahiri kwenye mitandao ya kijamii wakati walipocheza na Yanga na kutafunwa mabao 3 0 kuwa baadhi yao wanajiweka kando kwa sababu wana maslahi na Yanga, watarudi kwenye uongozi baada ya mchezo huo.Jambo hili nilililaani sana siku ile na niliandika humu humu Jamiiforums kuwaponda viongozi makanjanja kama hao.

Leo huko Mwanza mnyama kafanyiwa sana vurugu ili wale viongozi waliotangaza maslahi yao Yanga wakati ule wawafurahishe watu wa jangwani.

Pamba ya kuizuia Simba kesho iko wapi? Minziro huyu huyu kanjanja aizuie Simba?

Simba na Pamba hawakuwa na mahusiano mabaya tangu miaka hiyo tunazijua hizi timu, leo watu wengi wa Mwanza waliovamia mpira wakiwemo viongozi ambao wana matumbo makubwa na mijezi yao ya Yanga.

Miaka ya 1990 Simba ilikuwa inasajili sana wachezaji wa Pamba kuliko timu yoyote ile, Yanga ilibahatika kumchukua beki wa kulia mkatili David Mwakalebela, Fumo Felician wakati Simba ilimbeba Deo Mkuki, Dan Mhoja, Alphonce Modest, George Masatu, Hussein Masha, Nteze John, Bitta John, marehemu Rajab Msoma, marehemu John Makelele nk.

Leo viongozi wa Pamba wenye unasaba na kujipendekeza kwa Yang wanaifanyia fujo Simba ili kuwaondoa mchezoni kesho? Shame on you.

Pamba mmefukuza kocha, leo mmemuokota Minziro ndio mkamsumbue Ateba, Ahoua, mbona vituko hivi.

Acheni mambo ya kitoto, vurugu hizo ni dalili kuwa mnatumika na wala sio vinginevyo, mnautoa wapi upinzani na Simba nyie, mbona nyie na Simba ni mbingu na ardhi?
Ndo nashangaa unalalamika nn wakati pamba na mikia fc ni ndugu nyie!yanga ndugu yake toto Africa ila nyie ndugu yenu pamba!sasa mnagombana nn nyie wanandugu aisee
 
Screenshot_20241121-232253.png

Screenshot_20241122-000753.png
 
Back
Top Bottom