BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Uchira, wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamekusanyika kulalamikia uongozi wa serikali ya Kijiji hicho, kudaiwa kuuza maeneo ya barabara pasipo kuwashirikisha, hali inayowafanya kukosa njia za kwenda kutafuta huduma za kijamii.
Chanzo: ITV
*****
Nimesoma hiyo habari ikanikumbusha mazingira ya mtaani kwangu na mitaa mingine mingi tu ambayo nimewahi kuishi.
Kwa ufupi tangu nakua hadi hapa nilipofika nimeona vingozi wengi wa Serikali za Mtaa wanajiona wao ni wadogo n ahata jamii zetu zinazowazunguka zinawachukulia poa hivyohivyo.
Katika maisha kuna wakati jinsi utakavyojiweka ndivyo ambavyo watu wanaokuzunguka watakavyokuchukulia. Asilimia kubwa ya viongozi wa mtaa wao kazi yao kuuza viwanja na kuchukua posho ndogondogo.
Leo hii tuna matatizo kama ya Panya Road lakini kiuhalisia viongozi hao wa Serikali za Mtaa ndio wanatakiwa kuwa watu wa kwanza kubainisha matatizo ya mitaa yao na pengine kujua wahusika au kutoa mwangaza jinsi ya kudili na vikundi kama hivyo.
Hiyo ni kwao kuwa wao ndio wanaojua mitaa vizuri na wanajua wakazi wao wote, kama kuna mtu mwenye mishe za ajabu ajabu ni rahisi wao kumjua.
Kwa ufupi niseme hatuwatumii vizuri, tunawachukulia poa sana na ndio maana kuna uchafu mwingi nao pia wanauacha kwa kuwa wanaona siyo jukumu lao.