BRN
JF-Expert Member
- Nov 18, 2013
- 5,188
- 6,633
Kwa kilichotokea na kufanywa na viongozi wa Simba dhidi ya kocha mzawa Mgunda ni ukosefu wa fadhila na shukrani. Mgunda aliichukua timu wakati mgumu sana na kwa kipindi chote alichokuwa na timu morali ya wachezaji iliimarika na timu ilibadilika sana.
Hivi nyie viongozi mmetumia kipimo gani kupima ufanisi wa Mgunda?!mbona alifanikiwa tu..hivi mmejuaje kama Mgunda asingeifikisha timu nusu fainali?! si mngesubiri msimu uishe.
Viongozi wangu wa Simba mmeonyesha dhahiri ushamba wa sisi wa Tanzania wa kuamini watu wa nje(weupe) Wana jipya gani? Hivi, ni lini tutaamini watu wetu wa ndani kama hawa akina Mgunda.
Kila kukicha tunalalamika kwamba timu zetu zimejaa walimu kutoka nje wakati sisi hatuna walimu wanaofundisha nje..tungemuacha Mgunda aonekane kupitia Simba labda ingekuwa fursa ya yeye kuonekana na timu za nje..waliaminiwa na timu zao za ndani akina Ibenge,Motsemane nk na baadae wakapata kandarasi kubwa tu lakini imani ilianza na timu zao za ndani.
Hivi sisi hadi lini hii kasumba itatuisha..kwa kipi kikubwa huyo kocha mpya amekifanya huko alikotoka..kuifunga Mazembe?!
Kwa kweli,nimehuzunishwa,nimefadhaishwa na hiki kilichofanyika.
Msimuone Mgunda anacheka vile lakini lile tabasamu linaficha vingi sana na sina wasi wasi hata wachezaji morali imeshuka na ile jana hata kingepangwa kikosi cha kwanza wangefungwa tu.
Vile vile, hata viongozi ndani ya timu hili linaenda kuwagawa.
Hata kama Simba kuna pesa sana ila ningekuwa mimi Mgunda jana ile ile ningekuwa nishaondoka zangu( umaskini jeuri)ila yote kwa yote maamuzi anayo Mgunda mwenyewe.
Nisiwachoshe sana ila nimeona tu niiteme hii nyongo ili angalau nafsi yangu itulie,ila inauma sana na itoshe kusema kwamba wafadhila wapundaka.