Viongozi wa Simba, Uwanja wa Mkapa umulikeni, Utopolo wakimalizana na Zalan tukausafishe vinginevyo tumekwisha Jumapili

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Nimepenyezewa na watu wangu kuwa mipango inafanyika Simba apoteze kwenye mchezo wake dhidi ya Bata Bullets siku ya Jumapili, kuna uchafu mkubwa umefanyika ili tuondoshwe.

Nashauri mchezo wa kesho ukiisha tusiingie kichwa kichwa, kuna balaa limefanyika na watu wa upande wa pili ili wao wafurahi na wameshafurahi lakini Jumapili sisi tufe kwa Wamalawi kama tulivyokufa kwa Wabotswana.

Shida viongozi wetu wa Simba wanapenda sana kupuuza mambo tukiwashauri, wanatuona sisi hatuna akili na wao ndio wana akili sana, hivi mm niliyeanza kwenda uwanjani kuiangalia Simba mwaka 1989 nawezaje kudharauliwa na Barbara ambaye amekuja Simba juzi tu na hajui machungu ya Simba ikifungwa.

Mdharau mwiba huota tende, Utopolo wakimaliza mechi yao wataufanya mchezo wa kuwa mgumu mno, mfano mzuri angalieni walipocheza na Azam FC, kesho yake tukapata wakati mgumu mno kwa KMC wakati KMC ni mtoto mdogo tu.

Chondechonde viongozi, niko chini ya miguu yenu, Jumapili tutatafutana hapa, nyie haya tu. Mnadhani kama natania lakini ukweli ndio huo, wanaofanya mipango hiyo wapo na wanaendelea na mipango yao ili tufe bao 3-1 tena.
 
Ni kwel hilo sikupingi mkuu game nyingi anazo cheza utohapo afu tukija kucheza sisi lazma tule za uso,viongozi wafunge mkanda
 
Wakati mnafungwa na Kaizer Chief au Juaneng Galaxy Siku Moja kabla Kuna timu iliwahujumu? Simba Ipo certified kwenye ushirikina barani Afrika imekua approved na CAF Sasa nini kina watisha!!
 
Nimepenyezewa na watu wangu kuwa mipango inafanyika Simba apoteze kwenye mchezo wake dhidi ya Bata Bullets siku ya jumapili...
Kama mashabiki wa mpira wanamawazo kama haya, safari bado ndefu.

Mnaleta imani potofu huku mkitaka Matola afukuzwe. Bado sana safari Mnayo
 
Lazima mfungwe kwa sababu akili yenu inawaza kuwa Mpira ni uchawi.. Shame on you.. na mwaka huu mkitoboa makundi club bingwa njoo uniita Mbwa nipo hapa natype..
Mmetuingilia fani zetu yani nyie kwa sasa mmekua vigagula
 
Mnakumbuka ile clip ya juma shaban ya msimu iliopita ilkimuonyesha akifukia kitu uwanjani ili simba ipoteze mechi siku inayofuata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…