Viongozi wa Simba walioruhusu jezi za msimu mpya kutoka huku kifuani kukiwa na neno "SANDA" watakuwa na matatizo ya kiakili

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2,753
Reaction score
12,932
Usinchoshe na Nsikuchoshe,Tusichoshane!

Kwanza nikiri ya kwamba Mimi ni shabiki wa kutupwa wa Young Africans

Nikiwa kama mdau wa soka na mpenda maendeleo ya mpira,nimekuwa nikivutiwa na namna ambavyo soka letu limekuwa likioiga hatua,licha ya kucharuana,kutaniana na hata kuzodoana lakini linapokuja suala ukweli bila shaka huwa tunaambiana ukweli,Ukweli mara zote ndiyo umekuwa ukizisaidia timu kubwa hapa nchini kupiga hatua.

Napenda kukiri ya kwamba,Jezi ya watani zangu Simba SC a.k.a Makolo/Madunduka za msimu mpya 2024/2025 ni nzuri na zenye kiwango,Tatizo nililoliona ni neno "SANDA" kwenye jezi hizo.

Nimepata mashaka kidogo kama kweli hizi jezi viongozi waliziona kabla hazijatoka au zimetolewa kinyemela na wao wakiwa hawajazikagua!,Hivi kama kweli umeikagua jezi unawezaje kuruhusu ikatoka ikiwa na neno lenye ukakasi?

Yawezekana kabisa bwana Sunderland alikuwa na nia njema lakini Nia yake njema si Kwa namna hii,huu ni uhuni wa waziwazi Kwa timu kubwa kama Simba!

Kila mmoja anaelewa neno "SANDA" ni Vazi rasmi la Marehemu anapokuwa akizikwa,Sasa inakuwaje wakaruhusu neno "SANDA" likae kwenye jezi?,Ina maana wao hawaelewi maana ya SANDA?,Je hawaoni kama linaweza likawaletea uchuro kwenye msimu huu wa ligi?

Kuna msemo wa kiswahili usemao "Majina huumba"

Kwanini Sunderland asingeandika jina bland yake lote?,Kwanini afupishe?,kama nilivyosema,yawezekana alikuwa na maana nzuri lakini akumbuke hii nchi ya kiswahili,Kuna maneno yawezekana yakawa na maana nzuri nchi nyingine lakini hapa yakawa na maana mbaya!

Mfano

Kuna Mchezaji mzuri sana Simba walikuwa wakimtaka,alikuwa akiitwa Somebody Kapumbu,bila shaka Simba waliacha kumchukua kwasababu ya neno "KAPUMBU",yawezekana neno hilo likawa na maana nzuri kwao lakini si kwetu!

Nakumbuka pia Kuna balozi aliteuliwa nchi fulani kuja kuiwakilisha nchi yake hapa kwetu,akiitwa Somebody Kakuma,yawezekana neno "Kakuma" nchini kwake kusiwe na TAABU lakini nchini kwetu inaleta maana mbaya,hivyo nadhani Kwa busara za Viongozi wetu wakaomba aletwe mwingine!

Halafu pia Sunderland kwani kuna ulazima gani kuweka jina lako kwenye jezi,nani hajui jezi Kwa Sasa anatengeneza Sunderland?,mbona huwa hatuoni jina la Sheria Ngowi kwenye jezi za Yanga,nani asiyejua Ngowi ndiye mbunifu wa jezi za Yanga?

Hivyo niwaombe Viongozi wa Simba ikiwezekana hizo jezi zisiendelee kuuzwa,kama hii ni Batch ya kwanza,basi Batch ya pili zikitoka zisiwe na neno hilo!

Mkiendelea kukaza fuvu sisi watani zenu kazi yetu ni kuendelea kuwatania tu hatutakuwa na namna!

Yangu ni hayo tu leo
 
with that simba fans will be cooked. in business perspective, he is looking for a brand name, he wants all in football wear business.

he will probably do the same with taifa stars jersey. I believe taifa stars should have given gsm the jersey tender.
 
Sandaland ndio kampuni inayobuni, kutengeneza na kuuza jersey za simba

Hakuna shida kuweka brand name yao kiufupi,,, watu mlivaa brand ya FILA leo mnaipondea sanda
 
Wewe ndo hamnazo, hayoo yako hatuyataki tengeneza jezi yako, usitupangie chakuandika kama umechangia chcht kwenye iyo jezii
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
wwwe ndo hamnazo, hayoo yako hatuyataki tengeneza jezi yako, usitupangie chakuandika kama umechangia chcht kwenye iyo jezii
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
sawa SANDA FC

Tarehe 8 hizo hizo SANDA ndizo tutawashusha nazo kaburini
 
Sandaland ndio kampuni inayobuni, kutengeneza na kuuza jersey za simba

Hakuna shida kuweka brand name yao kiufupi,,, watu mlivaa brand ya FILA leo mnaipondea sanda
Brand name ni Sandaland, sio SANDA.
 
Sandaland ndio kampuni inayobuni, kutengeneza na kuuza jersey za simba

Hakuna shida kuweka brand name yao kiufupi,,, watu mlivaa brand ya FILA leo mnaipondea sanda
Haujui maana ya brand wewe,brand ni Sunderland na sio Sanda,alafu Fila sio kampuni ya Tanzania Kwa hiyo haina tatizo kwao
 
Wanachukulia mambo poa. Tutaona watakao vaa hizo jezi.

Wengine tunaendelea na zile za msimu ulipita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…