Viongozi wa Simba wana mipango mizuri sana tatizo ni wasiowatakia mema wanauza siri

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Leo Try again amewaahidi tena Simba kuwa msimu ujao hawatakuwa wanyonge, ni kama alivyoahidi kwenye Mkutano Mkuu wa Simba kuwa Ubingwa msimu huu ni wetu halafu kila mtu anajua kinachoendelea.

Mna mipango mizuri sana na watu tunawaelewa shida kuna wale jamaa wanaojita marafiki watawaharibia tu, kuna mechi lazima wawapigishe shoti ili SGM atangaze tena ubingwa msimu ujao.

Mambo sio rahisi kama mnavyotaka kutuaminisha. Safari hii mkitudanganya na Ubingwa ukapotea msione tabu kuachia timu, Simba ni kubwa sana na wapo watu wengi wenye uwezo wa kuiongoza.
 
Binafsi nawachukia sana.Kila mchezaji mzuri wanayemtafuta,unakuta wamezidiwa kete na utopolo.
Sasa sijui wana sababu gani kutamba wakati wanabahatisha sana.
Badala ya kuchukua wachezaji Congo wanaenda Afrika magharibi!Hivi Afrika Magharibi mchezaji mzuri aache kwenda ulaya aje Simba kweli?
 
Eng. Hersi aliwapa code ambayo amkutaka kujishughulisha na kujua ina maana gani, aliwaambia kuvaa jeans zilizochanika isiwe kigezo cha kuwadharau na kuwaita wahuni bali zingatieni big brain iliyopo vichwani mwa hao watu ndiyo itaendelea kuwatesa miaka yote! Sasa hivi simba imebaki kwenye propaganda na kusajili wachezaji kutoka ligi dhaifu ya Rwanda wakati wenzao wametuliza vichwa kuwashusha wakina makabi lilepo wa Al hilal alafu ligi ikianza mashabiki wenu waanze kulia lia mara oooh bahasha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…