Viongozi wa TLS Mwanza wajiuzulu, Mwabukusi atoa tamko

Viongozi wa TLS Mwanza wajiuzulu, Mwabukusi atoa tamko

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Dalili ziko wasi kwamba TLS sasa imemshinda Mwabukusi. Kuna mpasuko mkubwa na viongozi wenzake wameanza kumkimbia.

Ukimuona Mwabukusi anavyowananga wengine, unaweza kudhani anaweza hata kujiongoza yeye mwenyewe

====

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) mkoa wa Mwanza wametishia kuandamana hadi Ofisi ya Jaji Mfawidhi Mkoa wa Mwanza iwapo ombi lao la kuitishwa kwa uchaguzi kujaza nafasi za viongozi wa mkoa huo walioandika barua ya kujiuzulu halitozingatiwa.

Mawakili hao 46, wamejaza majina na kusaini fomu maalum (Petition) ya kushinikiza uongozi wa TLS ngazi ya taifa kuitisha uchaguzi wa kujaza nafasi za viongozi walioandika barua ya kujiuzulu nafasi zao ngazi ya Mkoa wa Mwanza.

Viongozi wanaotajwa kuwasilisha barua ya kujiuzulu ni Mwenyekiti wa TLS Mwanza (Chapter Convener), Msafiri Aloys Henga, Makamu wake (Vice chapter convener), Marina Mashimba na Mweka Hazina (Treasurer) wa TLS Mkoa wa Mwanza, Angelo Nyaoro.

Alipopigiwa simu kujua sababu za kujiuzulu, aliyekuwa Mwenyekiti wa TLS Mwanza, Msafiri Henga amethibitisha kuchukua uamuzi huo huku akisema hawezi kutaja sababu kwa kile alichodai hayuko kwenye mazingira mazuri ya kuzungumzia suala hilo.

Kwa upande wake, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Mwanza), Marina Mashimba amesema alijiuzulu wadhfa huo Agosti 21, mwaka huu na kuwasilisha barua kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TLS.

Kwa upande wake, Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi, amekiri kuwa na taarifa ya viongozi hao kuachia ngazi huku akisema tayari imeundwa kamati maalum ya kufuatilia sababu zilizochangia viongozi wa Mwanza kuchukua uamuzi huo.

Awali, Wakili Steven Kitale aliieleza Mwananchi kuwa tayari wamejaza majina na kusaini fomu maalum (Petition) ya kushinikiza uongozi wa TLS ngazi ya taifa kuitisha uchaguzi wa kujaza nafasi za viongozi na isipofanyika hivyo wataandamana kwenda kwa Jaji Mfawidhi Mkoa wa Mwanza.


 
Dogo usiwe mbishi 😂😂
Jipakulie manyama hayo.
Screenshot_20241222-114300.jpg
 
Unaonekana mshamba sana wa siasa wewe.

Mtu akijiuzulu haimaanishi kwamba hakubaliani na uongozi uliopo madarakani.
 
Mwabukusi ni kichaa tu. Ni mwanaharakati anayeongoza Taasisi ya taaluma.

Ndio maana haaangaiki na matatizo na changamoto za Taasisi yake, kama ustawi wa mawakili, vishoka, poor financial management etc

Yeye Kila siku ni matamko ya kisiasa. TLS walilamba gharasa hapa.
 
Ni baada ya TLs ya Mwabukusi Kuhongwa Gari na serikali na mama Abduli
 
Back
Top Bottom