Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mzee Popo au Baba Popo wa Isevya Mtaa wa Kanoni ndiyo babu yangu mzaa baba.
Jina lake ni Salum Abdallah ingawa jina lake alilopewa na baba yake ni Rashid.
Alibadilisha jina baada ya kufungwa kwa kumpiga Mwingereza aliyetaka kumdhalilisha.
Alipotoka jela ili aweze kupata kazi na kuwa salama akabadilisha jina lake akawa Salum.
Salum Abdallah maisha yake ya siasa yanaanza Dar es Salaam katika miaka ya 1920 hadi 1947 akiwa mfanyakazi wa Tanganyika Railways.
Locomotive Shed ilipohamishwa Dar es Salaam na kupelekwa Tabora ndipo akahamia Tabora ambako aliishi katika utoto wake baada ya Vita Kuu ya Kwanza.
Yeye alizaliwa Shirati Bomani ambako baba yake Mwekapopo Samitungo Muyukwa alikuwa askari katika jeshi la Wajerumani.
Huyu Mwekapopo aliingia Tanganyika kutoka Belgian Congo amebeba bunduki kuja kuimarisha utawala wa Wajerumani chini ya Herman von Wissman wakati Wajerumani wanapambana na Abushiri na Mkwawa.
Babu yangu aliongoza migomo mitatu dhidi ya Waingereza 1947, 1949 na 1960. Huu mgomo wa 1960 ulivunja rekodi kwani ulidumu kwa siku 82 treni hazitembei wala meli na mabasi ya Railway.
Walikaa mezani na Waingereza na wakayamaliza.
Inasemekana ni mgomo huu wa 1960 ndiyo uliomtisha Mwalimu Nyerere akajua hawa viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanasikilizwa na wananchi kwa hiyo katika Tanganyika huru hawa watampa shida.
1953 babu yangu na wenzake pale Tabora walimtuma Germano Pacha TAA HQ New Street, Dar es Salaam awaeleze viongozi wa TAA kuwa wao wanakusudia kuanzisha chama cha siasa.
Pacha alionana na Abdul Sykes nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Abdul alimwambia awaambie Tabora kuwa wafanye subira kidogo si muda mrefu atawaita Dar es Salaam kuja kuasisi TANU.
Huwa siishiwi na maneno ninapowazungumza hawa wazalendo ambao wanahistoria wetu waliwapuuza wakawa hawako katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Nahitimisha kwa kusema kuwa baada ya TANU kuundwa 1954 mwaka wa 1955 Salum Abdallah na Kassanga Tumbo wakaunda Tanganyika Railways African Union (TRAU) Salum Abdallah akiwa Mwenyekiti na Kassanga Tumbo Katibu.
TRAU na TANU wakawa bega kwa bega kupambana na Muingereza kuidai Tanganyika.
Bahati mbaya sana Salum Abdallah na Kassanga Tumbo na viongozi wengine wa Vyama Vya Wafanyakazi baada ya uhuru kupatika walikamhatwa na kuwekwa kizuizini.
Salum Abdallah na Bilal Rehani Waikela walitumikia kifungo chao Jela ya Uyui.
Angalia picha: