Viongozi wa umoja wa madereva wa Mabasi Tanzania (UWAMATA) watoa kero zao, waomba mazingira rafiki ya kazi

Viongozi wa umoja wa madereva wa Mabasi Tanzania (UWAMATA) watoa kero zao, waomba mazingira rafiki ya kazi

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Viongozi wa Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania (UWAMATA) Waomba Mazingira Rafiki ya Kazi

Viongozi wa Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania (UWAMATA) wameiomba Serikali kuwawekea mazingira rafiki ya kufanya kazi zao ili kudumisha amani na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia sekta ya usafirishaji.

Akizungumza na vyombo vya habari tarehe 11 Machi 2025, Mwenyekiti wa UWAMATA, Majura Kafumu, ameiomba Serikali kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wadogo waliopo pembezoni mwa barabara wanapangiwa maeneo rasmi ili kupunguza hatari ya ajali na kurahisisha shughuli za usafirishaji.

Naye Katibu Mkuu wa UWAMATA, Abdallah Lubala, ameomba madereva waajiriwe kwa mikataba rasmi ili kuepuka visa vya kuachishwa kazi kiholela, jambo linaloathiri ustawi wao na usalama wa ajira zao.
 
Hongera Madereva piganieni haki zenu,lakini pia acheni wizi wa Dizeli.
 
Back
Top Bottom