Viongozi wa Yanga acheni siasa Pyramid hamuwajui kisoka

Viongozi wa Yanga acheni siasa Pyramid hamuwajui kisoka

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika viongozi wetu wa vilabu vya soka Tanzania ni wanasiasa kabisa.Kwa watanzania walio wengi Klabu ya Pyramid ya Misri ni klabu isiyofahamika lakini mara baada ya jana CAF kutoa ratiba ya michuano na Klabu ya Yanga kupangiwa kucheza na Timu ya Pyramid ya Misri baadhi ya viongozi wa Yanga wameibeza Klabu hiyo na kujinasifu kuifunga timu hiyo.

Watanzania mtakumbuka viongozi hao hao wa Yanga walituhakikishia kupindua Meza nchini Zambia dhidi ya Zesco matokeo yake ni kubamizwa goli 2-1 na kutupwa nje.

Nashauri uongozi wa Klabu ya Yanga wawe makini na kauli zao mpira wa karne hii ni tofauti sana sio ule wa ushirikina kama walivyozoea, Klabu za Misri ni klabu zenye uchumi mzuri hivyo zinaajiri na kusajiri Makocha na wachezaji wazuri tofauti na Klabu za Tanzania.
 
Wanawaaminisha mashabiki wao kwamba wanaweza wakifungwa tu mashabiki wakilalamika wanasema hao wanatumika, hapa Yanga wakubali wanakamilisha ratiba tu.
 
Kwahiyo wewe ulitaka viongozi watamke kuwa "Pyramid ni timu ngumu sana hivyo timu yetu ya Yanga imeshaaga mashindano
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kuna mchezaji kanunuliwa Bilion 20 klabu hiyo hiyo ya Pyramid
Wewe ndezi hufuatilii soka...Kwa taarifa yako hao ndio habari ya jiji la Cairo..gharama ya mchezaji mmoja unanunua Yanga yote na ukoo wa Zahera.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Tusubiri tarehe 27 tutajua nani bingwa wa yote
Pyramid timu ndogo sana hawajawahi kushinda hata kombe la kugombea kuku, wamepanda daraja mwaka jana ndio waifunge YANGA? YANGA hata wakicheza kikosi B hawafungwi na pyramid.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kuna mchezaji kanunuliwa Bilion 20 klabu hiyo hiyo ya Pyramid
Wakati huohuo Vyura wanataka kumlinganisha huyo na Molinga wa Tsh. Milioni20..WTF😂😂😂😂😂😂
 
kwa wazee wa kubet ndio tunazijua timu. hiyo team ukiwekeza pesa zako ondoa shaka kabisa anapiga anachakaza balaa
 
Hii ni team mbona ya kawaida sana Yan yanga akikomaa anaingia kwenye. Makundi cha msingi ni kuwasapoti hawa tu
 
Kwahiyo wewe ulitaka viongozi watamke kuwa "Pyramid ni timu ngumu sana hivyo timu yetu ya Yanga imeshaaga mashindano
Ndio lugha sahihi ili wachezaji watie juhudi kupambana sio kuwadanganya
 
jamani natamani yanga wafungwe 😊😊😊😆😆😆😆😆😆7-1
 
Back
Top Bottom