Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari,
Kama taifa ni vyema tukaishi kwa misimamo thabiti. Ni vizuri tukaanza kuwajibishana bila kuoneana aibu ili kuleta fundisho kwa vizazi vya sasa na vile vinavyokuja.
Napendekeza viongozi wafuatao washitakiwe haraka, maana wamelitia taifa hasara.
1. Waziri wa maliasili na katibu mkuu wa wizara ya maliasili.
Washitakiwe kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi.
Je, ilikuwa sahihi kutumia fedha kuhamishia wanyama Hifadhi ya Burigi-Chato huku hifadhi nyingi ambazo tayari zina wanyama wa kutosha zinakosa fedha za miundombinu bora?
Waliohusika wote wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi.
2. Mkurugenzi mkuu wa TAA
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege ( TAA) .
Huyu afunguliwe mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.
Aliidhinishaje fedha nyingi zikajenge Chato Airport ambayo hatukuwahi kuona impacts zake za kiuchumi hapo awali na kuacha kuboresha Viwanja vya mikoa ambavyo vilikuwa miaka mingi? Atuelezee je, backup ya gharama zilizotumika kuujenga ule Uwanja zitapatikanaje?
3. Mkurugenzi mkuu wa TRC.

Kwanini hajatumia trilioni 2 kuboresha na kufufua shirika la reli kwa kununua mabehewa na vichwa vipya, kukarabati njia na vituo vya reli na badala yake yametumika ma trilioni kutujengea reli ya mwendokasi ambayo yataathiri watoto wetu?
4. Waziri wa maji.
Mawaziri waliohudumu wizara hii kwa kipindi kirefu wafunguliwe mashitaka .
Waeleze kwanini wameshindwa kusambaza maji kwa wananchi kwa 100% wakati tuna maziwa, mito na bahari.
N.k