Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Kuna watu ndani ya mfumo wa Serikali na chama Tawala wameshaona wananchi si kitu. Leo wakisikia mtu mmoja kasema funga wanasifia, kesho wakisikia fungia wanaendelea kupiga makofi. Watu wa aina hii wameqafanya wananchi kukosa dira na mwelekeo kwa sababu leo wanawaambia wananchi kaeni hapa na msibughudhiwe,kesho wakiamka wanawaambia ondokeni hapa na wananchi wanatii...In longran watafika mahali watachoka kupokea hizi amri na hapo ndipo waonevu wanaolipwa salary na marupurupu watakapolazimika kuwaheshimu wananchi. Tunawayumbusha wananchi bila sababu, tujifunze kuomba utaratibu, tujifunze kusema no.
Leo hakuna meya au diwani au Mbunge anayewatetea wananchi, wote wamekaa kimya kwa sababu wanaamini amri zote za chama chao Tawala ni halali. Hakuna Mbunge Wala Diwani anayejitokeza kushirikiana na wananchi japo kutafuta maeneo mbadala. Wote Wapo busy kustarehe na familia zao wakisubiri msaada wa tume na Polisi 2025. Basi Kama mmeamua hivyo sawa