Viongozi wanaofaa na wasiofaa kuwa Marais mbeleni

Viongozi wanaofaa na wasiofaa kuwa Marais mbeleni

1. Humphrey Polepole: Kijana huyu ameonyesha uzalendo, misimamo na kutonunulika na hayumbishwi (ANAFAA)

2. Kassim Majaliwa: Licha ya utendaji mzuri alionao katika nafasi yake, lakini ameonesha udhaifu mkubwa wa kimisimamo hasa baada ya ujio wa Samia kama Rais (HAFAI)

3. Philipo Mpango: Ingawa naona kama anatumia busara nyingi mno na upole mwingi katika nafasi yake, lakini naona akishika Urais atabadilika (ANAFAA)

4. Josephat Gwajima🙁ANAFAA)

NB:Huko upinzani sijaona anayefaa,waliojaa naona kazi yao kulitabiria taifa mabaya tu.

Mimi mtoa mada ni CCM, tena timu Magufuli
Ila magufuli ameshakufa mbona unaabudu mfu. Kwanini usiwe timu Samia. Au sukum gang inakutesa. Mimi cc mzalendo
 
Another hilarious joke borne of mediocrity.

Hii kuamini kuwa kuna watu fulani ndio wanafaa kuongoza nchi hii huku uwanja wa kujitokeza umedhibitiwa kama kuba ya hazina (treasury vault) ya BOT, ni kielelezo cha ujinga mkubwa uliotughubika. Nchi ina watu wazima zaidi ya 30 m wenye talanta kibao.

Tunapeana ujinga kufikiri kwamba kuna kikundi cha watu wasiozidi 20 ndio wanastahili kuchambuliwa na kuchaguliwa uRais. Eti Rais anaandaliwa kwa miaka. Eti kuna deep state inayohusika. Eti wananchi hawawezi kuelewa haya mambo. IT’S ALL HOGWASH BS. Tunatafuta Rais kama masihi anayesubiriwa na taifa la wayahudi! Hata wao wliamua kuwa REALISTIC na kuacha na na porojo hiyo; wakaanzisha a secular democratic state of Israel.

Ndio maana hadi leo hii tumebakia kuwa banana republic bila mwelekeo. Mara Tanzania ya viwanda, mara miradi ya mkakati, mara tuko uchumi wa kati, halafu mara tunafufua na kufungua uchumi uliokuwa na hali mbaya sana, n.k.

Tanzania itakuwa na Rais na viongozi wa maana pale kura za wananchi ndizo zitakuwa zinaamua nani aongoze nchi. Na wananchi hao hao kupitia katiba, mahakama na Bunge watakuwa na uwezo wa kuwawajibisha viongozi wote pale wanapoamua. Hakuna njia ya mkato: PEOPLE’S VOTES MUST COUNT. Nje ya hapo tusahau ustaarabu na maendeleo; tuendelee na mafia state yetu mpaka mabaradhuli (in Jenerali’s voice) watakapotusaidia kurejea akili zetu.
Mkuu hata kama wananchi tukawa na uwezo wa kuamua,bado upuuzi utakuwa uleule kwa sababu huwa tunajikita kwenye ushabiki na chuki bila kujali facts.

Ki-ufupi wajinga wanawazidi werevu
 
Ila magufuli ameshakufa mbona unaabudu mfu. Kwanini usiwe timu Samia. Au sukum gang inakutesa. Mimi cc mzalendo
Kwani mbona akina YESU na MOHAMAD wanaendelea kuhusudiwa tu?
 
Nchii hii papara za kutaka Urais utadhani ni mashindano ya urembo.
 
Sema Tanzania Nchi ya ajabu usishangae pole pole au Gwajima kuchukua fomu ukiuliza CV yake eti alikataa chanjo ya Corona...
Hivi mkuu kwamba hujui cv za hawa watu!!?
Suala la chanjo lina options mbili(serikali yenye ndio imesema),wao wamechagua hiyo ya pili,huko ndio kupinga?
 
Mkuu hata kama wananchi tukawa na uwezo wa kuamua,bado upuuzi utakuwa uleule kwa sababu huwa tunajikita kwenye ushabiki na chuki bila kujali facts.

Ki-ufupi wajinga wanawazidi werevu
TZ wananchi hawajawahi kuchagua Raisi wanayemtaka, kinachofanyika ni kamati ya CCM inateua mtu wao then CCM wanaiba kura ndio uchaguzi wa TZ
 
Mkuu hata kama wananchi tukawa na uwezo wa kuamua,bado upuuzi utakuwa uleule kwa sababu huwa tunajikita kwenye ushabiki na chuki bila kujali facts.

Ki-ufupi wajinga wanawazidi werevu
Hakuna mbadala wa wananchi katika nchi yao. Wananchi wanayo haki ya kuamua viongozi wao wenyewe. Wana haki ya kukosea na kusahihisha makosa yao kupitia nguvu ya kura zao. Mwaka 2016 Marekani walimchagua Donald Trump kuwa Rais wao. Mwaka 2020 walimpiga chini kwa kura baada ya kutoridhika na mwenendo wake wa kuchochea ubaguzi nchini.

Kama Watanzania ni wajinga, ni nani huyo miongoni mwao anayekubalika kama mwerevu mwenye dhamana ya kuwaamulia Watanzania Rais wao? Kwa vigezo gani? Hata wewe binafsi huwezi kukubali kuamuliwa umuoe nani au ufanye kazi gani. Kukosea katika kuchagua ni sehemu ya changamoto za maisha, sio mwisho. Uhuru na demokrasia ya kweli vinakupa fursa ya kuweka sawa mambo yako pale inapobidi. Sio kikundi kidogo cha watu wenye hulka za kimafia kinaamua mustakabali wa watu milioni 60.
 
Hakuna demokrasia ya namna hiyo.
Huyo trump mwenyewe ushindi wake ulilalamikiwa na wamarekani,watu walimtaka Hilary ila mfumo ulimtaka trump
 
Upeo mdogo wa fikra ni mbaya sana

kila anayepinga serikali anaonekana anafaa kuwa rais

huyuhuyu pole pole aliyekua anapiga mna na vieite kwa nchi masikini ambayo hadi leo umeme, maji, elimu, Afya na miundombinu Bado Iko chini…. Huyuhuyu aliyekua anacheza mayenu huku ukawa wanapiga kelele za uonevu

gwajiboy… huyu huyu aliyetukana waislamu, na wakatoliki kwenye public , huyu aliyekua Kwenye ile video ya kuanzisha taifa la waislamu?

vijana mnatakiwa mtafute forum humu jf iwe inawapa shule ya historia ya tulipotoka, aina za uchumi tulionao, uwanda mzima wa siasa, katiba na dira za vyama

Pia tuwe na forum ya kuangalia sifa muhimu za potential presidential candidates

rais haokotwi, rais anaandaliwa
Kama poyoyo anafaa Basi sema kijani wote wanafaa.
 
Hakuna demokrasia ya namna hiyo.
Huyo trump mwenyewe ushindi wake ulilalamikiwa na wamarekani,watu walimtaka Hilary ila mfumo ulimtaka trump
Hakuna huo ujinga wala porojo za mfumo.

Mwaka 2016 Trump alichaguliwa kwa kura (electoral college votes) nyingi kumzidi Hillary na 2020 aliangushwa kwa kura hizo hizo (electoral college votes) nyingi zilizoenda kwa Biden. Watu kulalamika ni ada lakini wanatambua ukweli na mambo yanasonga. Hizi talalila za "mfumo" mwisho wake ni kwa misukule huku banana republics.
 
Popular votes Hilary alimpiga chini Trump,na popular votes ndio maamuzi ya wananchi.
 
Back
Top Bottom