Viongozi wanaofaa na wasiofaa kuwa Marais mbeleni

Ila magufuli ameshakufa mbona unaabudu mfu. Kwanini usiwe timu Samia. Au sukum gang inakutesa. Mimi cc mzalendo
 
Gwajiboy ataweka kitimoto kama kitoweo rasmi cha Taifa
 
Mkuu hata kama wananchi tukawa na uwezo wa kuamua,bado upuuzi utakuwa uleule kwa sababu huwa tunajikita kwenye ushabiki na chuki bila kujali facts.

Ki-ufupi wajinga wanawazidi werevu
 
Ila magufuli ameshakufa mbona unaabudu mfu. Kwanini usiwe timu Samia. Au sukum gang inakutesa. Mimi cc mzalendo
Kwani mbona akina YESU na MOHAMAD wanaendelea kuhusudiwa tu?
 
Nchii hii papara za kutaka Urais utadhani ni mashindano ya urembo.
 
Sema Tanzania Nchi ya ajabu usishangae pole pole au Gwajima kuchukua fomu ukiuliza CV yake eti alikataa chanjo ya Corona...
Hivi mkuu kwamba hujui cv za hawa watu!!?
Suala la chanjo lina options mbili(serikali yenye ndio imesema),wao wamechagua hiyo ya pili,huko ndio kupinga?
 
Mkuu hata kama wananchi tukawa na uwezo wa kuamua,bado upuuzi utakuwa uleule kwa sababu huwa tunajikita kwenye ushabiki na chuki bila kujali facts.

Ki-ufupi wajinga wanawazidi werevu
TZ wananchi hawajawahi kuchagua Raisi wanayemtaka, kinachofanyika ni kamati ya CCM inateua mtu wao then CCM wanaiba kura ndio uchaguzi wa TZ
 
Mkuu hata kama wananchi tukawa na uwezo wa kuamua,bado upuuzi utakuwa uleule kwa sababu huwa tunajikita kwenye ushabiki na chuki bila kujali facts.

Ki-ufupi wajinga wanawazidi werevu
Hakuna mbadala wa wananchi katika nchi yao. Wananchi wanayo haki ya kuamua viongozi wao wenyewe. Wana haki ya kukosea na kusahihisha makosa yao kupitia nguvu ya kura zao. Mwaka 2016 Marekani walimchagua Donald Trump kuwa Rais wao. Mwaka 2020 walimpiga chini kwa kura baada ya kutoridhika na mwenendo wake wa kuchochea ubaguzi nchini.

Kama Watanzania ni wajinga, ni nani huyo miongoni mwao anayekubalika kama mwerevu mwenye dhamana ya kuwaamulia Watanzania Rais wao? Kwa vigezo gani? Hata wewe binafsi huwezi kukubali kuamuliwa umuoe nani au ufanye kazi gani. Kukosea katika kuchagua ni sehemu ya changamoto za maisha, sio mwisho. Uhuru na demokrasia ya kweli vinakupa fursa ya kuweka sawa mambo yako pale inapobidi. Sio kikundi kidogo cha watu wenye hulka za kimafia kinaamua mustakabali wa watu milioni 60.
 
Hakuna demokrasia ya namna hiyo.
Huyo trump mwenyewe ushindi wake ulilalamikiwa na wamarekani,watu walimtaka Hilary ila mfumo ulimtaka trump
 
Kama poyoyo anafaa Basi sema kijani wote wanafaa.
 
Hakuna demokrasia ya namna hiyo.
Huyo trump mwenyewe ushindi wake ulilalamikiwa na wamarekani,watu walimtaka Hilary ila mfumo ulimtaka trump
Hakuna huo ujinga wala porojo za mfumo.

Mwaka 2016 Trump alichaguliwa kwa kura (electoral college votes) nyingi kumzidi Hillary na 2020 aliangushwa kwa kura hizo hizo (electoral college votes) nyingi zilizoenda kwa Biden. Watu kulalamika ni ada lakini wanatambua ukweli na mambo yanasonga. Hizi talalila za "mfumo" mwisho wake ni kwa misukule huku banana republics.
 
Popular votes Hilary alimpiga chini Trump,na popular votes ndio maamuzi ya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…