Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,222
- 2,912
Japokuwa kauli ya Makamu wa Rais baadhi ya watanzania hasa wanaharakati wanaiona kama ni kauli ya kishujaa na kuwahamasisha wananchi wanaodai katiba mpya kutokata tamaa
Hata hivyo ni kauli yenye mashaka na inayotakiwa kuchambuliwa kwa ubongo wa ndani
Kuna maswali kadhaa ya kujiuliza hapa;
1. Wanaotoa kauli tata kuhusu katiba mpya ni viongozi wa CCM akiwemo Rais aliyewahi kusema katiba ni "kijitabu". Halafu leo anakuja mwenzao anasema "wapambanie katiba mpya" bila kusema wanatakiwa kupambana dhidi ya nani?
Je, anajua kuwa "wao" hawako tayari kuwapa wananchi katiba mpya?
2. Kuna watu wametaja taja swala la katiba mpya lakini sasa hivi wengine ni marehemu, wengine hawajulikani walipo, wengine wako gerezani.
Anataka watanzania gani wapambane? Hao waliokutwa na yaliyowakuta hawakuwa watanzania?
3. Kwanini swala la katiba mpya hadi liwe mapambano?
Viongozi hawaoni umuhimu wake?
Wanafurahia namna katiba iliyopo inavyowaminya wananchi?
Ni hayo tu kwa sasa