Viongozi wanaswa kwenye msako wa Dawa za kulevya

Viongozi wanaswa kwenye msako wa Dawa za kulevya

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa kukamata kilo 1,983.31 za dawa za kulevya na kuteketeza ekari 55.5 za mashamba ya bangi katika operesheni kabambe ya mwezi Machi 2026.

Katika msako huo uliofanyika nchi nzima, watuhumiwa 77 walitiwa mbaroni huku vyombo vya usafiri ikiwemo magari tisa na pikipiki 12 vikikamatwa vikitumika kusafirisha shehena hizo.

Takwimu zinaonyesha ongezeko la usafirishaji wa mirungi, ambapo zaidi ya kilo 1,200 zilikamatwa zikiwa zimefichwa kwa mbinu za kisasa.

Miongoni mwa matukio makubwa ni ukamataji wa mirungi ndani ya mfumo wa hewa (AC) wa basi la abiria jijini Dar es Salaam, pamoja na dawa nyingine zilizofichwa kwenye mabelo ya nguo na magunia ya maembe mikoani Mwanza na Tanga.

Operesheni hiyo imewanasa pia baadhi ya viongozi wa kijamii, akiwemo Diwani mmoja mkoani Arusha na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa mkoani Tanga, wakihusishwa na usafirishaji wa dawa hizo.

Aidha, mamlaka imebaini kuingizwa kwa dawa za kulevya aina ya 'skanka' kwenye makazi ya wanafunzi jijini Dar es Salaam, jambo linaloashiria mabadiliko ya mbinu za walanguzi kulenga taasisi za elimu.

Sambamba na hayo, kiasi kikubwa cha kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya kilizuiliwa ili kuzuia uchepushwaji unaoweza kutumika kuzalisha dawa za viwandani.

Serikali imesisitiza kuendelea na doria kali na kutoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano ili kudhibiti mitandao mipya ya wahalifu bila kujali nafasi zao katika jamii.

Soma pia

1776146869044.png

Chanzo: ITV
 
Hivi huko kusini kuna jina la mbong almaarufu kama"party" ushalisikia huko dizonga
Isanga family

Ova
 
Hivi huko kusini kuna jina la mbong almaarufu kama"party" ushalisikia huko dizonga
Isanga family

Ova
Hapana sijamsikia mkuu miaka ya sasa hivi hatuishi kama zamani yaani unaweza kuwa SA wanaojua ni wale ambao unafanya nao kazi tu na labda ikitokea misiba kwenda kuchangia zile mambo za zamani kuwa pamoja kwa story na ishu zingine zisizo na mpango sasa hivi hakuna..
 
Ah ok

Ova
 
Back
Top Bottom