Parabora
JF-Expert Member
- Jul 6, 2019
- 1,504
- 2,203
Nasema hili nikiwa nimeliona katika ofisi nyingi za serikali baada ya kurudi likizo huko nyumbani, Serikali inatumia gharama nyingi sana kulipa mishahara na posho za watumishi lakini ni wachache sana, wachache mno wanaofanya kazi, wengi wao wanaripoti na kupiga soga mda wote wakiwa kazini ilimradi tu wamefika kazini na wamesaini na pengine sio kwamba wanapenda ni kutokana na ubovu wa sera na mifumo yetu, kiukweli mifumo mibovu ya serikali inachangia kwa kiasi kikubwa hii hali.
KWA NINI NASEMA HIVI
Kuna baadhi ya kada (vitengo) katika taasisi za umma kwa ofisi nyigi ambazo nilibahatika kuzitembelea havina majukumu tena lakini watumishi wake bado wanaendelea kuwepo na wanalipwa mshahara bila hata kufanya kazi yoyote kwa kipindi chote wanachokuwa hapo. Mfano: Labda taasisi A kipindi inaundwa ilikuwa na uhitaji wa watu wa masoko kulingana na maboresho na mabadiliko ya taasisi husika, kitengo hicho hakihitajiki tena kwenye muundo wa taasisi hiyo na kinavunjwa lakini watumishi wa kada yake wanaendelea kuwepo bila majukumu huku wakila mishahara bila kufanya kazi.
Wao wanafika na kusaini tu then wanaendelea na majukumu yao bnafsi, wakati kuna sehemu taasisi nyingine kuna uhitaji wa kada hiyo, kwanini hizi taasisi wasiwe wanawasiliana na utumishi wawapangie sehemu zenye uhitaj?
Ukitembelea taasisi za serikali kuna rasimali watu hazitumiki ipasavyo huku wakiwa wanakula mishahara kama kawaida, na wengine wamekuwa frustrated kutoka na roho mbaya za viongozi wao wasiokuwa na karama za uongozi. Just imagine mtumishi anataka kubadilisha kituo ch kazi kutoka mkoa A kwenda mkoa B ofisi hiyo hiyo na ana sababu za msingi kabisa badala ya kusikilizwa anapuuzwa na anapotelekeza majukumu yake chini ya kiwango anawekwa benchi huku mshahara anaendelea kupata na stahiki zake zingine. Hapa viongozi waliopewa madaraka ya kusimamia hizi taasisi huwa inamkomoa nani?
Just Imagine, serikali imefuta kada ya ulinzi katika taasisi zake nyingi za umma na tenda wamepewa SUMA JKT, lakini wale walinzi walioajiriwa wapo na hawana majukumu wanaingia ofisini wanachati tu na kupiga story mda wote na mda wa kuondoka ukifka wanaondoka ama wanatumika katika majukumu wasiyoyamudu kiasi kwamba hawaleti ufanisi unaotakiwa, huwa najiuliza kwa nini utumishi isingewasambaza hawa security katika taasisi zinazohitaji hiyo kada kama TPA, KADCO, TAA, TANAPA, UDSM, MUHAS, SUA na kwingineko ili wakaongeze nguvu kuliko kulipwa mishahara huku wakiwa hawana kazi za kufanya, Ukiangalia bandari zipo nyingi ukiachana na ya Dar, Tanga na Mtwara zipo za Kigoma, Mwanza, Rukwa, Bukoba, Geita, Musoma na kwingineko.
Na viwanja vya ndege vipo vingi karibia kila mkoa na hata watumishi wa kada hiyo hawatoshi ni wachache hali inayopelekea kuwa na usalama duni hasa kwenye airport nyingi, TANAPA kwenye hifadhi ndio usiseme kwa nini hawa watu wasiende kuongeza nguvu huko kuliko kuwalipa mishahara bila kutekeleza majukumu yao, yaani mtu anaenda kazini kupiga stori tu na umbeya unamlipa mshahara. Utumishi inaweza kuwa ni wizara mbovu kabisa hapa nchini, yaani unalipa kada ya ulinzi mara 2 kwa SUMA JKT wanaofanya kazi na walioajiriwa ambao hawana tena majukumu yao ya kufanya huku wakiwa kwenye payroll.
Kuna haja hata ya kuwahamisha walimu walioomba uhamisho walio na sababu za msingi kabisa kwenda kwenye vituo walivyoomba, kuwakatilia ni kuwatengenezea msongo wa mawazo na hata kazi za kufundisha hawatafanya kwa ufanisi.
Sio mwandishi mzuri, lakini ninachojaribu kusema serikali ina mfumo mbovu sana inalalamika haina watumishi wakati huohuo vijana wako mtaani hawawaajiri na wengine wametelekezwa bila majukumu wanakula mishahara ya bure wakati wangeweza kutumika sehemu zenye uhitaji na wakaongeza ufanisi na sijui kazi ya Wizara ya Utumishi wa Umma huwa ni nini hasa?