Parabora
JF-Expert Member
- Jul 6, 2019
- 1,504
- 2,203
- Thread starter
-
- #21
Mkuu maoni yako ni mazuri mno, kwa ninavyojua ofisi nyingi sasa zina punching machine za kusign in and out.Ni kazi rahisi sana kuongeza ufanisi Serikalini na kwenye mashirika ya umma basi ndio vile tu tunapenda kuchekeana na kusaidiana saidiana siku ziende maana maisha yetu haya tunafahamiana.
TANZANIA NI NCHI MASIKINI SERIKALI IANGALIE UWEZEKANO WA KUONGEZA MASAA YA KAZI WATU WAANZE KAZI SAA KUMI NA MBILI NA KUTOKA SAA KUMI NA MBILI JIONI KWA MAANA YA MASAA KUMI NA MBILI KWA SIKU.
- Kila ofisi lazima iwe na biometric machine kwa wafanyakazi kupunch in and out.
- Kila ofisi lazima iwe na Job Card ambazo kila mtu anapewa asubuhi ajaze masaa aliyofanya kazi na kazi husika.
- Tupunguze ajira za moja kwa moja, baadhi ya kazi ziwe kwa masaa na watu walipwe kwa masaa waondoke.
- Kila bosi kila ofisi apewe target na kuwe na mfumo wa kumuasses na kujiasses mwenyewe.
- Kila Mfanyakazi kila mwaka awe assesed mara mbili mpaka tatu kwa mwaka.
- Tea break iwe nusu saa na wawe wanapunch out and in na huo uwe muda wao sio wa mwajili GOVT.
- Lunch time iwe lisaa limoja na usiwe muda wa mwajili na punch in and out kama kawaida.
- Masaa ya kazi manane kuanzia saa mbili mpaka saa kumi na moja na nusu plus ule muda wa kula lisaa na nusu.
- Baadhi ya vyeo marufuku kuendeshwa lazima ujiendeshe mwenyewe hapa dereva tunamtoa.
BARABARA ZOTE ZIFAGILIWE USIKU NA WAFAGIAJI WALIPWE KWA MASAA, MAHOSPITALI YOTE YA UMMA YAFAGILIWE USIKU NA WAFAGIAJI WALIPWE KWA MASAA..
Sasa tatzo ni hapa kwenye assessment kama unavyosema, kwa mfano idara ya Estate imefutwa na Kuna watumishi bado wapo na ni maengineer by professional, na mshahara anakula na allowance huku akiwa hana majukumu.. hapa utamfanyia vipi assessment wakati majukumu yake tayari hayapo kwenye taasisi?
Hawa walinzi ambao mheshimiwa raisi aliagiza serikali isiajiri tena na badala yake watumie wa kampuni ya SUMA JKT, still waliokuwa wameshaajiriwa wako wanakula mshahara ila hawalindi wanalinda wa kampuni ya Suma... Huyu utamfanyia vipi assessment wakati majukumu yake hafanyi? Au kapangiwa majukumu ambayo haendani nayo ana anaperfom chini ya kiwango utamchukulia hatua?
Hapa solution ilikuwa ni kupelekwa sehemu watakazofanya kazi za kada zao....
Umri wa kustaafu miaka60 bado naona sio mbaya mengine yote uko sawa kabisaa mkuu