Wenye mawazo mbadala huwa wanahesabiwa sio wenzetu hivyo hutengenezewa kashfa na mizengwe mingine ya kuwafifisha ili wasisikike tena !!Wa kurehemu,kusujudiwa ni Mungu baba pekee
Shida tunaishi na tunafanya mambo yetu kwa mazoea.kila mwaka hali ni ile ile miaka nenda rudi.hakuna ubunifu wala ugunduzi.hakuna mawazo ni namna gani ya kukabiliana na upungufu wa nishati ama maji kuepuka mgao na kukatakata.
Hatukai hata tukatafuta mbadala.
Tumeozea.kikubwa mishahara inaingia basi mengine yarajisolve yenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu mpaka wamefunga salon zao kwa upuuzi wa TANESCONi busara sana kuomba kusamehewa pale ambapo umekosea. Watanzania kulalamikia upatikanaji hafifu wa maji safi kwenye mabomba na kukatika katika kwa umeme naona ni kosa kubwa na hatustahili kuiomba serikali iboreshe huduma hizi muhimu kwa jamii.
Malalamiko haya yamekuwa ni kelele kwenye masikio ya baadhi ya watu. Yatupasa kuwaomba hao watu msamaha kwa kuwapigia kelele.
Kwa upande mwingine, tunaomba mturehemu kwani sisi pia tunahitaji huduma hizo muhimu kuishi, kujitafutia kipato na hivyo kuyafanya maisha yetu kuwa ya furaha.
Najua mnaweza kutoa rehema hizi kwetu na tutawasujudia na kuwaimbia nyimbo za sifa.