Viongozi wetu wa Dini acheni kutuchanganyia siasa na dini

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
8,598
Reaction score
9,539
Kwa unyenyekevu mkubwa nawaomba viongozi wangu wa dini wasitumie madhabahu kama majukwaa ya kisiasa kwani waumini tunao Sali ni wafuasi wa vyama mbalimbali hivyo matamko na misimamo ya kivyama yanatugawa na kutuchanganya sisi waamini.

Chondechonde nawaomba viongozi wangu wa kidini waendee masuala ya kisiasa kwa HEKIMA na BUSARA ikibidi basi zitumike njia ambazo haziwagawi waumini.

Kama tutatumia MAKANISA na MISIKITI kama machimbo ya kupanga mikakati ya kisiasa basi tutaliangamiza Taifa letu lakini pia tutakuwa tunapanda chuki kwa vizazi vijavyo katika kila vipindi vya utawala wa Taifa letu.
Nawasilisha.
 
Na nyie viongoz muache kuapa kwa kutumia biblia
Nitatumia Biblia kuuapa ila ninacho kisema ni viongozi wangu wa kidini WASITUMIKE kisasa kwani watatugawa, tutashindwa kufanya ibada....wanapaswa walifahamu hilo.
 
Tulieni sindano iwaingie, mlitaka mtukuzwe na wanyonge wakandamizwe. Hao ndio viongozi wa ukweli sio wale wala bata kule jumba jeupe lenye utukufu wa kisiasa
 
mtu kama Kalikawe Bagonza na huyu Kitima mkabila hawewezi kuelewa ukweli huo mtupu gentleman 🐒
 
Mmmh kwani kuna kiongoz wa dini kataja chama chochote au kasema anajihusisha na chama fulani, vp kuhusu mwamposa uliwahi anzsha thread kama hii khs maneno yake ya kujihusisha na siasa au hamtaki skia haki ila mnataka skia amani tu
 


Haki haina Chama . Haki ya binadamu popote inahitaji kufuatwa kwa sheria .

Kanisa ni ufalme wa Mungu duniani na hayo ya kwenu HAYAWEZI KUWA JUU YA KANISA MiLELE Amina .
Hata Roman Empire ilishindwa kuliangusha Kanisa ikabidi ijichanganye na Kabisa .

Hatuhitaji uchaguzi wa dhulma halafu Jeshi la Wananchi likaliwe na fisadi aliyechaguliwa na wananchi .

Mwaka huu mtanyooka na dhulma zenu . No Reforms no Election,
Rasilimali za nchi hii sio mali ya wazanzibari peke yao chini ya Chama cha mapinduzi . Kila mTanzania ana haki sawa na mwingine . Hakuna haki ya CCM kuonea wengine kisa Raisi ni amiri Jeshi mkuu .
Mkitaka watoeni na wakuu wote wa vyombo vya dola wenye kumwamini Mungu mbaki na machawa wa kuua watanzania wenzao kwa sababu ya vyeo na maslahi ya watu wachache walioshiba na kutapika mali za umma .
Kupuuza waraka wa kanisa Katoliki ni kupuuza ukristo.
Kudharau ma baba askofu wa kanisa katoliki ni kudharau kanisa duniani kote .Kuwanyanyasa wakristo na kuwabagua ni kumbagua kristo mwenyewe. Kuwaua wakrsto ni kumuua Kristo mwenyewe , kutowasikiliza maaskofu wa kanisa ni kutomsikiliza Kristo na kutowasikiliza wakristo.

Kanisa litakuwa limefanya makosa makubwa sana kama litakaa kimya na kuacha mifumo yenye dhulma kutamalaki na kuzoeleka na kuonekana kama kawaida .

Hatutakubali kabisa kuona uchaguzi wa kuwatumia polisi watoto wa maskini kuwaua watu ili Bilionea mmoja , mama Abdul ashinde kwa dhulma halafu watoto wa maskini wabaki na maumivu na njaa.

Nimesikiliza Hotuba zote za viongozi wa dini ya Kikristo hakuna hata mmoja aliyesema kuwa Watu wasiende kupiga kura wala wetu wasichague au wamchague mtu fulani .
Wote wameongeza habari za kukaa pamoja na kuweka maridhiano, ukiona hivyo basi waumini wao wengi wamechoshwa na chaguzi za kisanii halafu watu wanauana kwa sababu tu kuna kundi halitaki haki na kufuata sheria .

CCM Imewaharibu mpaka BAKWATA ambayo ni taasisi ya dini . Leo Bakwata ni waoga wa kutaja neno Haki . Wanaona ukosema neno haki unamkwanza Rais na CCM. Wanataka kuhalalisha dhulma kwenye nchi . Haiwezekani Bakwata nchi nzima wote ni CCM ya dhulma . Mashekhe kwa mamia walifungwa gerezani kwa miaka mingi na serikalli ya CCM bila kosa halafu leo wamambosw kuwe haki sawa kwa wote kni muhimu sana.

Dhulma ikitawala nchi watu wote wanaonja joto ya jiwe
 
Unawasilisha wapi? Na wewe eti great thinker
 
Uko sahihi kabisa
 
Nitatumia Biblia kuuapa ila ninacho kisema ni viongozi wangu wa kidini WASITUMIKE kisasa kwani watatugawa, tutashindwa kufanya ibada....wanapaswa walifahamu hilo.
Hivi sisiem nanyi huwa mnafanya ibada kwa Mungu yule wa mbinguni kabisa!?

Kweli dunia ina maajabu🤔
 
Nasisitiza hizi ni KAULI ZA KISHETANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…