Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Hivi tangu lini ukamuona msemaji wa Serikali wa Marekani anasimama na kuanza kuchamba raia au wafanyakazi wengine?
---------------------
Nimesikiliza speech ya Msigwa jana yaani amenikera alichokuwa anataka kukiwasilisha kilikuwa ni kina maana lakini uwasilishaji ni sifuri. Hata kama ni maafisa wa serikali alitakiwa kuja na official document aseme kosa kisheria na adhabu anayotakiwa kupewa mtu atakayevujisha siri za serikali na anayetumia mitandao vibaya aondoke zake.
Nashangaa amekazana mara watoto wa maskini, mara "hawana mbele na nyuma". Watumishi wa serikali na viongozi wapatiwe training ya public speaking na wafundishwe etiquettes. Maana hata bunge nako uwasilishwaji wa hoja ni sifuri na limegeuka bunge la vichambo na hiki ni kizazi cha wasomi.
Nimesikitika kuona Baba Levo anampita Msigwa ambaye anajinadi ni nguli wa taaluma ya Habari kwenye uwasilishaji wa taarifa kwa umma.
Kuna vitu vidogo tunavipuuzia lakini baadae vinakuja kuzua matatizo makubwa na taharuki.