Viongozi zungumzeni ukweli

Viongozi zungumzeni ukweli

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
“Tanzania ni moja ya Nchi 12 zitakazozindua mpango mahususi wa kitaifa kuhusu nishati, kupitia mpango wetu tunatarajia kuongeza kasi ya kuunganisha umeme nchini hadi kufikia 72% ifikapo mwaka 2030, ili kufanikisha azma hiyo ndani ya muda wa miaka mitano ijayo, tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 13, ambapo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi hapa nchini.”

“Kupitia mpango huu tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko, Tanzania ni kiungo muhimu katika kuunganisha umeme Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na hivyo kuwezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Misri, tayari tumeunganisha miundombinu ya umeme na Nchi za Burundi, Kenya na Rwanda na sasa tunaendelea kuunganisha miundombinu ya umeme na Nchi ya Zambia na Uganda”

“Kuwepo kwa miundombinu hiyo kutawezesha biashara ya nishati kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme ikizingatiwa kuwa hadi November 2024 mahitaji ya umeme Tanzania yalikuwa megawatt 1888 wakati uzalishaji wetu mi megawatt 3431”
1738086087612.jpg


“Muelekeo wetu ni kufikisha umeme katika vitongoji vyote 64359 baada ya kufanikiwa katika vijiji vyote vya Tanzania, hadi sasa tumevifikia vitongoji 32827 na kazi inaendelea katika vitongoji vilivyobakia , la nne ambalo mpango huu utafanya ni kusambaza nishati safi ya kupikia” ——— Rais Samia akiongea kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika leo January 28,2025 Jijini Dar es salaam.

-------------------------------------------
Rai yangu:
1. Tanzania na watu wengi tunaishi kwenye dunia ya taarifa hakuna kitu watu ndani ya Tanzania ambacho hakifahamiki, uwezo wetu wa kuzalisha umeme na kusambaza umeme unajulikana. Anachokizinguza Samia kinaweza kuwa ni sawa na hadithi ya Mpishi ambaye anakula Mara moja kwa siku akimpa ahadi mtoto wa mtaani kuwa atampa milo mitatu kwa siku, ni uongo?

2. Viongozi wajifunze kuongea noble lies zinazoeleweka sio matusi, kama treni ya umeme tu zinazima zikiwa kwenye safari je kuuza umeme nje tunaanzia hatua gani? Hapa team mapambio wanaweza kusifia kwa nguvu kisa tu Samia ameongea! Ni unafiki kabsa.

3. Wahenga wanasema kabla hujarekebisha kuti la nyumba ya jirani basi hakikisha fito za nyumba yako ipo imara. Sio siri usambazaji wa umeme kupitia chombo cha TANESCO kimekuwa ni moja ya kituko kikubwa, sio kwa maneno ya Msigwa wala Samia, tunaambiwa uongo na wanajua wanazungumza uongo.
 
Jambo la muhimu ni kuendelea kufuatilia utekelezaji wa mpango huu na kuhakikisha kwamba viongozi wanatueleza ukweli kuhusu maendeleo yake
 
Jambo muhimu ni kuendelea kufuatilia utekelezaji wa mpango huu na kuhakikisha kwamba viongozi wanatueleza ukweli kuhusu maendeleo yake
Unaongea ukweli pasipo hitajika ukweli.
 
Back
Top Bottom