Watuhumiwa wa EPA waponda raha Keko
2008-11-13 10:21:29
Na Joseph Mwendapole
Washitakiwa 18 wanaokabiliwa na mashitaka tofauti ikiwemo kughushi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wanaishi katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko tofauti na mahabusu wengine.
Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa, baadhi ya washitakiwa hao wamewekwa katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko ambapo wametengwa kabisa na maabusu wa kawaida maarufu kama walalahoi.
Chanzo cha gazeti hili kilielezwa kuwa, Jayantkumar Patel maarufu kama Jeetu Patel na Jonson Lukaza, wanaishi katika vyumba vya VIP, ambapo Jeetu Patel inadaiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu huku Lukaza akidaiwa kuwa na maradhi kama hayo pia.
Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omari Mtega aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu jna kuwa, katika magereza yote hapa nchini, hakuna vyumba vya VIP.
Kamishna Mtega alisema ni jukumu la Magereza kuhakikisha ulinzi na usalama wa wahalifu hivyo ni muhimu walindwe kwa utaratibu waliojiwekea.
Aliongeza kuwa, jamii nzima inawachukia watuhumiwa wa EPA hivyo jeshi hilo haliwezi kufanya uzembe kwa kuwachanganya na watuhumiwa wa makosa mengine.
``Unasikia mwandishi, `EPA is EPA`kwa hiyo sio jukumu la vyombo vya habari kujua usalama wa watuhumiwa na wanalindwaje na hatuwezi kuwachanganya na watuhumiwa wengine kwa kuwa wanaweza wakauawa na lawama zikaenda kwa jeshi,`` alisema.
Aliongeza kuwa, mahabusu ambao ni watuhumiwa sugu kwa makosa tofauti, hawachanganywi na wale wanaofikishwa gerezani kwa mara ya kwanza.
``Kwa mfano, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watuhumiwa gerezani, jeshi haliwezi kufanya makosa kwa kuwachanganya na Abdallah Zombe kwa sababu wanaweza kumdhuru au hata kumuua hasa wale waliokamatwa kwa tuhuma mbalimbali kabla Zombe hajakamatwa kwa tuhuma za mauaji,`` alifafanua Kamishna Mtega.
Baadhi ya masharti ya dhamana ambayo wamekuwa wakipewa ni pamoja na kulipa nusu ya fedha wanazodaiwa kuiba BoT au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Sharti lingine ni kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali, kuwasilisha hati za kusafiria na kuripoti polisi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi na kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila kibali cha Mahakama.
Hivi karibuni, gazeti moja liliripoti kuwa, serikali ilikuwa ikifanyia ukarabati vyumba vya VIP kwa ajili ya vigogo waliotarajiwa kufunguliwa mashitaka kutokana na wizi uliotokea BoT.
Hata hivyo, baada ya taarifa hizo, serikali ilikuja juu na kukanusha kuwa ukarabati huo haufanywi kwa ajili ya vigogo bali ni taratibu za kawaida wamewekwa katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko ambapo wametengwa kabisa na mahabusu wa kawaida maarufu kama walalahoi.
Chanzo cha gazeti hili kilielezwa kuwa, Jayantkumar Patel maarufu kama Jeetu Patel na Jonson Lukaza, wanaishi katika vyumba vya VIP, ambapo Jeetu Patel inadaiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu huku Lukaza akidaiwa kuwa na maradhi kama hayo pia.
Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omari Mtega aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu jna kuwa, katika magereza yote hapa nchini, hakuna vyumba vya VIP.
Kamishna Mtega alisema ni jukumu la Magereza kuhakikisha ulinzi na usalama wa wahalifu hivyo ni muhimu walindwe kwa utaratibu waliojiwekea.
Aliongeza kuwa, jamii nzima inawachukia watuhumiwa wa EPA hivyo jeshi hilo haliwezi kufanya uzembe kwa kuwachanganya na watuhumiwa wa makosa mengine.
SOURCE: Nipashe